Sunday, 20 April 2014
Kundi la P-SQUARE lasambaratika ....Je!!! unakijua chanzo.....soma hapa full stor.......!!!!!!
Ni siku chache tu zimepita toka Paul Okoye wa kundi la P-Square afanye harusi ya kimila na mke wake Anita Isama huko Nigeria, lakini baada ya wote wawili (Peter & Paul) kukamilisha majukumu ya ndoa zao, kuna habari ambazo zimesambaa wiki hii kuwa umeibuka ugomvi baina ya mapacha hao wa kundi la P-Square ambao inasemekana sasa hawaelewani vizuri.
Mtandao wa Naija Gists umeripoti kuwa kwa mujibu wa chanzo, inadaiwa kuwa kumekuwa na kutoelewana baina ya kaka mkubwa wa mapacha hao Jude Okoye na mke wa mdogo wake Peter Okoye aitwaye Lola Omotayo, kitu kilichopelekea Jude kutohudhuria harusi yao mwaka jana.
Kama unakumbuka Jude hakuhudhuria harusi ya Peter na Lola mwaka jana, lakini alihudhuria ya Paul na Anita mwaka huu kitu kinachowafanya watu waamini kuwa kuna tatizo kubwa baina yao.
Chanzo hicho kimesema inadaiwa kuwa ugomvi huo unaomhusu Lola umesababisha Peter na Paul kugombana wakati wako kwenye rehearsle Jumatano wiki hii, mpaka walipoachanishwa na dancers wao.
Kaka mkubwa wa P-Square Jude alitweet kitu ambacho kinaaminika kuwa kinahusiana na ugomvi wao.
“After over 10 years of hard work, it’s over. (I) Am done.” ikiaminika kuwa alimaanisha amejiondoa kuli-manage kundi hilo japo kuwa yeye mwenyewe hakufafanua alichomaanisha katika maneno hayo machache.
After over 10yrs of hard work, it's over. Am done.
— IG: @Judeengees (@judeengees) April 18, 2014
Jude ndiye amekuwa akiwa-manage kwa miaka yote na kuproduce hits zao pamoja na kudirect idadi kubwa ya video zao zilizofanya vizuri.
Lakini kuna baadhi ya watu nchini Nigeria wamedai kubwa kuna uwezekano kuwa ugomvi ‘hewa’ unaoendelea na kuripotiwa katika vyombo vya habari ukawa ni ‘hype’ ya kuandaa ‘kiki’ ya album yao mpya
Endlea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kujua kitakachojiri kuhusu kundi la P-Square
Related Posts:
Oscar Pistorius jela Miaka 5 Pistorius alipatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake bila kukusudia Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuu… Read More
Essien akana kuugua Ugonjwa wa Ebola Baada ya kuripotiwa kuugua ugonjwa wa EBOLA - hatimaye kiungo wa kimataifa wa Ghana Micheal Essien amejitokeza na kusema yeye ni mzima wa afya - hajaathirika na ugonjwa huo.… Read More
Msanii Y.P wa kundi la TMK Wanaume Family afariki dunia.MENEJA wa kundi la TMK Wanaume Family aliye pia mkurugenzi wa MKubwa na Wanae, Said Fella 'Mkubwa' amethibitisha kuwa msanii YP amefariki dunia usiku wa kumakia leo. Akizungumza na BantuTz hivi punde kwa njia ya simu, F… Read More
Baraza la Sanaa (BASATA) kumvua taji miss Tanzania 2014 kwa udanganyifu juu ya umri wake Sakata la lililojitokeza la mrembo wa Taifa wa mwaka huu 'Redd's Miss Tanzania 2014', Sitti Mtemvu kudaiwa kudanganya umri, limeingia katika sura mpya baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kueleza kuwa litamvua taji hil… Read More
Uthibitisho kuhusu nyimbo mpya ya Ali Kiba 'aliyomchana' Diamond Baada ya kutokuwepo kwa maelewano huku vyombo mbalimbali vya habari nchini vikiripoti bifu/ugomvi unaoendelea kati ya nyota wawili wanaotamba katika mziki wa bongo fleva nchini;Diamond na Ali Kiba.Leo hii BantuTz imek… Read More
0 comments:
Post a Comment