Sunday, 20 April 2014
Unaijua sababu ya Marehemu Gurumo kupoteza Jicho lake moja...............fuatilia hapa kujua sababu hiyo...................
Marehemu Gurumo kwa maisha yake yote alikuwa na ulemavu wa jicho moja lakini hakuna mwanamuziki wala mdau au mwanahabari aliyekuwa anajua sababu ya madhila hayo ya mzee wetu mpendwa.
Gurumo akaileza Saluti5 mbele ya mdau mkubwa wa muziki Juma Mbizo sababu ya jicho lake kupotea.
Ilikuwa jambo la kusisimua sana. Alitupeleka hadi mbele ya nyumba yake na kukutana na mti wa mwembe na kisha akasema: “Leo nataka niwaambie jambo moja ambalo sijui kama yupo mtu anayelijua.
“Huu mti una historia kubwa kwangu. Hapa ndipo nilipopoteza jicho langu nikiwa na umri wa miezi mitatu.
“Mama yangu alinilaza kwenye kivuli cha mti huu kisha akaenda kuendelea na shughuli zake. Bahati mbaya likaanguka tawi na kutua kwenye jicho langu.
“Nilisimuliwa kuwa juhudi za hospitali hazikusaidia kitu, nikapoteza jicho langu,” alimaliza Gurumo na kisha akataka arekodiwe kwa njia ya video ili tujipatie kumbukumbu adimu.
Baadae tutakuwekea video ya Gurumo akisimulia namna alivyopoteza jicho lake
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kufamau mambo mengi ya wasanii yaliyojificha....................
Related Posts:
Uthibitisho kuhusu nyimbo mpya ya Ali Kiba 'aliyomchana' Diamond Baada ya kutokuwepo kwa maelewano huku vyombo mbalimbali vya habari nchini vikiripoti bifu/ugomvi unaoendelea kati ya nyota wawili wanaotamba katika mziki wa bongo fleva nchini;Diamond na Ali Kiba.Leo hii BantuTz imek… Read More
Utambue ujangiri unaofanywa kupitia akaunti za facebook Habari zenu wadau wa BantuTz... Mataifa hivi sasa yanapambana vikali na CYBER CRIME ambapo hivi karibuni IRAN wamevipiga vyombo vya usalama vya MAREKANI attack kwa computers ambazo zinakuwa kwa ajili ya Ulinzi na Us… Read More
Steve Jobs is Apple Inc,Apple inc is Steve Jobs "iGenius" Binadamu tunaamini maisha ya mwanadamu hubadilika kutokana na mazingira,lakini mazingira hayo yanamtegemea mwanadamu kwa namna moja au nyingi,inamaana hivi ni vitu viwili vinavyotegemeana,Mwanadamu anayategemea mazingira na… Read More
Will Facebook be Free or Under PAYMENTS?Kuna stori ambayo tuliripoti ambayo inavutia sana juu ya Mtandao Nguli wa Kijamii FACEBOOK kuwa Utaanza kulipiwa na wote wataotumia??? Kunaweza kuwa na ukweli ama si kweli lakini kama wanaTEKNOLOJIA hebu tujadili apa. … Read More
Nyuma Ya Pazia Kuzama kwa Meli Ya Titanic-Sehemu Ya Pili Naam matajiri wote walishaingia ndani ya Meli wakiongozwa na John Jacob Astor ambaye kama nilivyosema hapo awali huyu ndiye alikuwa bilionea namba 1 duniani kwa wakati huo, Hakuna yeyote aliyejua kwamba Meli hii ya ki… Read More
0 comments:
Post a Comment