Facebook

Tuesday, 22 April 2014

Manchester United yathibitisha kumtimua kazi David Moyes, Giggs na Nicky Butt kushika hatamu.......fuatilia hapa....................


 1560414_715196531877628_3796186308205047484_n
giggs

Hatimaye kocha Manchester United David Moyes amefukuzwa kazi, miezi 10 baada ya kumrithi Sir Alex Ferguson.
United jana waligoma kuthibitisha kuhusu ripoti kwamba Moyes angefukuzwa mwishoni mwa msimu.
Moyes, 50, alichaguliwa na Sir Alex Ferguson kumrithi wakati kocha huyo mwenye 72, alipoamua kustaafu baada ya miaka 26 mwaka jana baada ya ligi kuisha.
Moyes aliondoka Everton na kusaini mkataba wa miaka sita na mabingwa ya Premier league.
Kwenye taarifa rasmi, klabu ilisema: “Tungependa kumshukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya, uaminifu wake aliokuwa nao kwenye kazi yake”.
Ryan Giggs kwa pamoja na Nicky Butt watashika majukumu ya ukocha mpaka mwishoni mwa msimu.


Related Posts:

  • Makala:Maneno yanauma kuliko meno...    Cristiano Ronaldo alipokuwa mtoto, aliwahi kumpiga mwalimu wake na kiti kwa sababu alimtania kwa lafudhi yake ya Madeiran, Mourinho aliwahi kumuita Wenger Master of failure! Tuachane na hayo..Guardiola alifikish… Read More
  • :Ni ndoto tu..... Je Unadhani Hawa Jamaa Ipo Siku Watakuja Kucheza World Cup Na Euro Au Watashia Kuangalia Kwenye Tv Kama Shujaa Wao wa Nchi ile Ryan Giggs Na Majembe Mengine Ya Zamani ya Nchi ile kama Akina Ian Rush, Bellamy,… Read More
  • Mambo muhimu usiyoyajua kuhusu Atletico Madrid Athletico Madrid imeonekana kuwa maarufu kwa baadhi ya wapenda soka hasa Tanzania katika siku za karibuni kutokana na kufanya vizuri kwenye la liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini hii timu ni bora tokea muda… Read More
  • NIFIKIRIAVYO:Yaya Toure na makombe yake, Hazard-Suarez na tuzo zao Karne ya 6 kabla ya kuzaliwa Kristo Generali wa China na mtaalamu wa mbinu za jeshini anayejulikana kama Sun Tzu aliandika kitabu “the art of war” sehemu ya maneno kwenye kitabu hicho muhimu sana kwenye jeshi la Uchina wak… Read More
  • MAPATO KWA VILABU LIGI KUU UINGEREZA MSIMU 2013-14 Klabu zina njia kuu 3 za kujipatia kipato:- 1. mapato ya mechi - viingilio, kuuza chakula na vinywaji na nk 2. mapato ya kibiashara - shati wazamini, mikataba ya vifaa mbalimbali, bidhaa 3. mapato vyombo vya habari - televi… Read More

0 comments:

Post a Comment