Facebook

Saturday 22 November 2014

SERIKALI YAHAMIA DODOMA, PINDA NA KAGASHEKI WATOLEANA UVIVU

Hali sasa ni dhahiri si shwari tena mjini Dodoma.Pilikapilika za magari ya vigogo pamoja na ndege ndivyo vinavyotawala kwa sasa katika mabarabara na uwanja wa ndege!

Katika hali ambayo si ya kawaida, vigogo wa ngazi za juu wa CCM pamoja na serikali wameingia Dodoma kwa fujo hivi leo huku makamu wa rais dr. Mohamed Gharib Bilal akitarajiwa kutua hapa mchana wa leo tayari kuongoza kikao kutokana maelekezo aliyopewa na rais Jakaya Kikwete.

Jana waziri Prof. Mark Mwandosya aliitwa Dar kwa dharura na tayari amerudi Dodoma leo asubuhi na mapema akiongozana na vigogo wakuu wa CCM wakiwemo Kinana na Mangula.

Katika tukio jingine mbunge Hamisi Khagasheki amejikuta katika mtifuano mkubwa na wanaomuunga mkono Pinda baada ya kumtuhumu waziwazi waziri mkuu Pinda katika mitandao ya kijamii kuwa ni mwizi ambaye hakupaswa kusubiri hadi leo.

Miongoni mwa waliomjia juu Khagasheki ni John Komba huku akimdhihaki kuwa anaona gere baada ya kutoswa uwaziri!

CCM hapa Dodoma imepasuka vibaya sana kwani kuna wakati Pinda anazomewa waziwazi na wanaCCM wenzake wakiwamo wabunge hali inayoashiria kuwa sasa uwaziri mkuu wa Pinda umefikia tamati!
Bado hali ni ngumu na inaelekea dr. Bilal anakuja na ujumbe kutoka kwa rais Kikwete.Pia tayari imethibitika kuwa zote hizo ni jitihada za kumnusuru Pinda ingawa Werema, Tibaijuka Muhongo, Masele na Maswi watalazimishwa kwa mara nyingine kujiuzulu leo. Hawa wote wameambiwa iwe isiwe ni lazima wang'oke kabla ripoti haijapelekwa bungeni!

0 comments:

Post a Comment