Facebook

Sunday 23 November 2014

Boko Haram lauwa watu 100 Nigeria.

Ripoti kutoka kaskazini-mashariki mwa
Nigeria zinaarifu kuwa kundi la wapiganaji
Waislamu la Boko Haram, limefanya
mashambulio mawili makubwa katika siku
chache za karibuni ambapo watu karibu 100
wameuwawa.

Kiongozi mmoja katika jimbo la Borno alisema
kuwa wapiganaji waliuwa wauza samaki karibu
50 karibu na kijiji cha Doron Baga, kando ya
Ziwa Chad.

Alisema wapiganaji wa Boko Haram wameweka
kizuizi kwenye njia ya kuelekea Chad na
kuwakamata wachuuzi waliokuwa wakienda
kununua samaki.

Katika tukio jengine hapo awali watu karibu 50
waliripotiwa kuwa waliuwawa karibu na mpaka
wa Cameroon pale Boko Haram walipovamia
kijiji cha Azara Kuya, siku ambapo soko huwa
na watu wengi.

0 comments:

Post a Comment