Facebook

Saturday 19 September 2015

Mh.Lowassa aanza kampeni mkoa wa Kagera,aahidi neema kwa wakulima.

Mh.Lowassa hapo jana alianza ziara mkoa wa Kagera kwa kishindo na kuahidi neema kwa wakulima.
Mgombea urais wa UKAWA Mh Edward Lowassa ameingia kwa kishindo katika mkoa wa Kagera na amesema akichaguliwa kuwa rais mikoa yenye uhakika wa uzalishaji ukiwemo wa kilimo inapewa kipaumbele kinachostahili na wakulima wanapewa mikopo ya kuanzia miaka 5 hadi 15 na wanakuwa mfano wa kuigwa katika kupambana na umaskini.

Mh Lowassa jana alifanya mikutano katika majimbo ya Kerwa Karagwe, Muleba kusini na Muleba kaskazini.

0 comments:

Post a Comment