Facebook

Sunday 20 September 2015

Mbowe:Uteuzi wa wagombea majimbo Ulizingatia vigezo vyote.

Mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi nchini Tanzania UKAWA Bw. Freeman Mbowe amesema uteuzi wa wagombea wa ubunge katika majimbo kwa kushirikisha umoja huo ulizingatia uwezo wa mgombea husika na sifa alizokuwa nazo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mbowe amewataka wale wanaolalamika kwamba wameonewa kuacha kufanya hivyo kwa kuwa tathmini ilishafanyika na kuonekana kwamba wao hawana uwezo wala sifa za kupewa majimbo hayo.

Amesema katika UKAWA hakuna mtu atakaeonewa eti kwa sababu tu zisizo na msingi bali atachaguliwa kutokana na uwezo wake na matakwa ya wananchi hivyo wale wote ambao hawakuchaguliwa hawajaonewa bali uwezo wao umenekana ni mdogo.

0 comments:

Post a Comment