Facebook

Saturday 19 September 2015

Wakala "Ozil anaweza kuondoka mwishoni mwa msimu huu"

Dr Erkut Söğüt ambae ni wakala wa Mesut Ozil ametoa maneno ambayo yamewashtua watu wengi labda hasa mashabiki wa Arsenal. Wakala huyo akiongea na vyombo vya habari vya Uturuki alizungumzia uwezekano wa mchezaji wake kuhama Arsenal mwisho wa msimu huu.

Dr Erkut Söğüt alisema, “Tusubili nini kitatokea mwisho wa msimu, kama akihama Arsenal chaguo lake ni Fenerbahce. Mwisho wa siku hii ni club kubwa na kwa sasa ina mipango mikubwa. Imekua ikisajili wachezaji wazuri na inafaa kwa mchezaji wangu. Lakini kwa sasa ni mapema sana kuzungumzia kuhusu mambo ya uhamisho”

Fenerbahce imemsajili Robin Van Persie akiwa kwenye miaka 30 lakini Ozil bado ana miaka 26, bado ana nafasi ya kuendelea kucheza kwenye club kama Arsenal au kwingine ambapo kuna damu changa.

0 comments:

Post a Comment