Facebook

Friday 18 September 2015

Huyu ndiye Mahrez anayempa jeuri kocha wa Leicester City na Kuwanyima Usingizi mabeki Ligi Kuu Uingereza

Claudio Ranieri ameanza kutajwa sana kama Meneja aliyerejea kwa kasi kwenye EPL na kuanza kutishia uhai wa timu ndogo ambazo ziliamini Leicester City na Sunderland ndio wahanga wa kuteremka daraja hivo wao hawatokuwa na shaka kumbe sivyo. Leicester wameanza vyema na uwezo wao unachagizwa na kiwango kikubwa cha kijana mmoja wa kiarabu ambaye alionekana kwenye kombe la dunia pale Brazil. Kijana huyu amekuwa sio anatoa assist pekee bali anafunga magoli yanayoihakikishia timu yake uhakika wa pointi 3. Leo naomba tumtazame Riyad Mahrez,winga ambaye ndiye anayekusudiwa hapa.
Alitumia muda mwingi kucheza kwenye timu ya vijana ya mtaani kwake ya AAS Sarcelles kabla ya mwaka 2009 kuanza kucheza soka la kulipwa kwenye timu ya Quimper, kwa sasa timu hii ipo ligi daraja la 4 pale Ufaransa. Pia Le Havre ambayo ipo French Legue 2 ilimchukua na hapa ndipo Leicester City walipomuona na kumpa kandarasi ya kudumu. Akiwa Ufaransa Mahrez alitupia magoli 32 katika michezo 147 huku akitengeneza magoli ya kutosha kwa washambuliaji wa timu alizopitia.
Mahrez alianza kuonesha makucha yake tangu Leicester ikiwa chini huku
akiwa miongoni mwa walioipandisha timu hii daraja.
Magoli 4 aliyoyafunga kwenye mechi za ufunguzi na kiwango chake cha kutisha, vimemfanya atajwe kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi. Sio rahisi kuaminiwa na kutajwa kwenye tuzo hii kwani kuna wachezaji wenye viwango vikubwa kwenye EPL. Japokuwa tuzo hii ilichukuliwa na kijana kutoka Ghana, ila naamini Mahrez naye alistahili kuingia kwenye kinyang’anyiro.
Mwazo wake mzuri unefanya jina lake kuongeza umaarufu na hata Ufaransa kujuta kwanini hawakumuita kwenye timu yao ya vijana kipindi cha nyuma kwani kwa sasa wangekuwa na ‘Asset’ ya uhakika kwenye taifa lao.Kiwango kikubwa walichokionesha Algeria kwenye michuano ya kombe la dunia iliyopita kilichagizwa na viwango vikubwa vya Wa-algeria akiwemo Riyad Mahrez.
Kutokana na uwezo wake wa kupiga vyenga na kasi ya kutisha kule pembeni, ni jambo la kheri kwa kijana huyu kwani amekuwa ni miongoni mwa wachezaji 5 katika zile ligi kubwa ambao wanaongoza kwa kufanya ‘Dribbles’ mara kibao. Baada ya Lionel Messi, Neymar, Alejandro Gomez na Serey Die wa Stuttgart, Mahrez ndiye anayefata akiwa na wastani wa ‘kudribble’ mara 4.4 kwa kila mechi. Hakuna mchezaji mwingine kutoka EPL mbali na Mahrez.
Kutokana na kiwango na mwenendo wake ni wazi kuwa Riyad Mahrez anaelekea pazuri na huenda jina lake likawa kubwa pale Algeria na kuwafunika akina Nabeel Bentaleb, Islam Sliman na Yacine Brahimi. Nina wasiwasi msimu ujao Mahrez anaweza kulihama jiji la Leicester na kwenda kutafuta maisha katika vilabu vingine vikubwa kidogo tofauti na Leicester city. Pia usishangae kuona anachukua tuzo za mwezi kibao kwenye EPL au hata zile za ndani ya klabu yake. Pia tuzo za nyota wa mchezo hazitoacha kumuangukia kama atakuwa na mwenendo huu wa kuridhisha.

0 comments:

Post a Comment