Facebook

Friday 18 September 2015

NINACHOKIAMINI MAESTRO:UCHAMBUZI CHELSEA vs ARSENAL.

Na: Ayoub Hinjo (Ayo's Mata Maestro).

CHELSEA vs ARSENAL

1: ULINZI

CHELSEA:  Chelsea ndio timu iliyoruhusu magoli mengi kwenye ligi kuu kuliko timu yoyote(Magoli 12). Hii inaonyesha ni jinsi gani ukuta wa Chelsea umekuwa mwepesi kupitika. Defensive error zimekuwa nyingi sana hasa upande wa kulia anaocheza Ivanovic mara kwa mara,upande huo umetumiwa sana na wapinzani kama sehemu dhaifu zaidi ya ulinzi ya kikosi cha Chelsea.

ARSENAL:Arsenal wao wanaonekana wana ngome imara ya ulinzi kuliko Chelsea,imeruhusu magoli machache(Magoli 3) tu. Utofauti wao unaweza kuanzia hapo kwenye ulinzi. Arsenal wanaonekana imara kuliko Chelsea.

2: KIUNGO

CHELSEA:Ukilinganisha na msimu ulioisha kiungo cha Chelsea kilionekana kigumu kupitia hasa pale anapokuwepo Nemanja Matic kwenye kiungo cha ulinzi na Fabregas kwenye kiungo cha kushambulia lakini sasa imekuwa kinyume kulinganisha na msimu wa mwaka jana. Tumeshuhudia Mourinho amekuwa akitumia viungo wawili wakuzuia ili kuleta uwiano wa timu inapokuwa ina mpira au haina mpira.

ARSENAL: Kijana tegemezi wa mzee Wenger kwenye eneo la kiungo cha kuzuia,Conquelin ana imara kila siku inayoitwa leo. Anapevuka kiakili ni tofauti na alivyokuwa kwenye nafasi hiyo mwaka jana. Hapa nilikuwa namzungumzia mchezaji bora wa mwezi wa kikosi cha Arsenal. Mseto wa Cazorla na Conquelin unazidi kuwa mtamu kila siku zinaposogea,timu ya Arsenal imekuwa na uwiano mzuri wa kuzuia na kushambulia. 

3: USHAMBULIAJI

Kwa timu zote mbili tatizo kubwa limekuwa kwenye umaliziaji au eneo la mwisho la kumalizia kazi. Chelsea imefunga magoli 3 tu na Arsenal imefunga magoli 5 tu. Hakuna tofauti sana kati yao. Kwa nini washambuliaji hawafungi vya kutosha!!? Hapa kuna mambo mawili labda yameshindwa kutumiwa ipasavyo na washambuliaji. Either nafasi zinatengenezwa chache kwenda kwao au nafasi zinatengenezwa za kutosha lakini wanashindwa kuzitumia vyema.

HITIMISHO:

Kasi waliyonayo wachezaji wa Arsenal inaweza kuleta tatizo kwenye timu ya Chelsea. Hasa kasi ya washambuliaji wa Arsenal inaweza kuwa kikwazo kikubwa kwa beki za Chelsea. Kasi ya wachezaji wa Chelsea haijakaa sawa bado na hii imechangiwa na kutumia nguvu nyingi kushinda makombe ya Capital One na Ligi kuu msimu ulioisha.

Timu itakayotumia nafasi vyema itaondoka na ushindi kwenye mchezo huo. Natoa credit kwa Arsenal.

0 comments:

Post a Comment