Facebook

Thursday, 24 September 2015

Barcelona yapokea kichapo La-Liga.

Barcelona walipokezwa kichapo chao kikubwa zaidi La Liga wakiwa chini ya Luis Enrique baada ya kulazwa 4-1 na Celta Vigo Jumatano.
Kushindwa huko kulifikisha kikomo mapema rekodi yao ya kushinda mechi zao zote msimu huu.
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Iago Aspas alifunga mawili baada ya Nolito kuanza ufungaji mabao dhidi ya klabu hiyo yake ya zamani.
Neymar alikomboa moja upande wa Barca zikiwa zimesalia dakika 10 mchezo kuisha, kabla ya nyota wa zamani wa Manchester City na Stoke John Guidetti kufungia wenyeji bao la nne.
Barcelona walikuwa wamepoteza mechi moja pekee kati ya 25 walizocheza majuzi zaidi La Liga.
Ushindi wa Celta uliwaweka kileleni mwa ligi kwa muda, lakini Real Madrid waliwabandua baadaye baada ya kulaza Athletic Bilbao.
Mkufunzi mkuu wa Barca Luis Enrique, alisema: "Kilichoamua mechi hii ni jinsi Celta walivyocheza. Walicheza vyema sana.
“Tulijaribu kuwatatiza lakini walituzidi ujanja. Timu inapokuwa bora kukushinda, huwa huna mengi ya kusema.
"Heri nishindwe na timu inayocheza kama Celta walivyocheza leo, bila kutumia hila, kushinda kwa kucheza vyema soka. Nawapongeza na natumai waendelee kucheza vivyo hivyo.”
Hiyo ilikuwa mara ya tatu kwa Barca kufungwa magoli manne katika mechi tisa walizocheza msimu huu.
Walilazwa 4-0 na Athletic Bilbao katika Super Cup ya Uhispania na pia walicharaza Sevilla 5-4 katika Super Cup ya Uefa.

Related Posts:

  • Klabu ya Lille yawasilisha rasmi ofa ya kumsajili Samatta.Klabu ya Lille inayoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa imewasilisha rasmi ofa ya kumsajili mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC) na Taifa Stars, imefahamika. Katika mahojiano na moja ya vituo vya televisheni vya Afrika Kusini usiku … Read More
  • Matola aachia ngazi Simba SC.Kocha msaidizi wa simba Suleiman Abdallah Matola amejiuzulu nafasi hiyo kutokana na kile alichodai kutolelewana na Kocha Mkuu, Muingereza, Dylan Kerr. Matola amesema kwamba amefikia uamuzi huo baada ya kuona maelewano na bosi… Read More
  • MEMPHIS DEPAY NA MIPANGO YA KURUDI KWENYE KIWANGODepay: "Khali Ni Ngumu Unapokuwa Benchi,Lakini Ni Nzuri Kwa Sasa Na Itakuwa Nzuri Mazoezini Pia. Kwahiyo Nikipata Nafasi Ya Kucheza.,Nitaitumia" Depay: "Mambo Mengi Yamebadilika.,Niko Kwenye Klabu Mpya Kwa Sasa, Na Ligi Ya Ki… Read More
  • Sepp Blatter alazwa baada ya mshutuko. Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa, Sepp Blatter amelazwa hospitalini kutokana na kupatwa mshituko wa neva. Blatter aliyesimamishwa kwa siku 90 kujishughulisha na masuala ya soka wakati akichunguzwa kwa kashfa za rushwa … Read More
  • Suleiman Matola aachia ngazi Simba SC.Kocha msaidizi wa simba Suleiman Abdallah Matola amejiuzulu nafasi hiyo kutokana na kile alichodai kutolelewana na Kocha Mkuu, Muingereza, Dylan Kerr. Matola amesema kwamba amefikia uamuzi huo baada ya kuona maelewano na bosi… Read More

0 comments:

Post a Comment