Mhudumu mmoja wa bustani ya kuhifadhi wanyama ameuawa na chui mwenye milia huko Hamilton New Zealand.
Kupitia kwa kwa mtandao wao wa twitter bustani hiyo ya kuhifadhi ya wanyama ya Hamilton ilisema kuwa
''Tunasikitika kuwa tumempoteza mmoja wa wahudumu wetu wa bustani ya wanyama baada ya kushambuliwa na chui mwenye milia kutoka Sumatra.''
''kwa sasa tunaendelea kutoa msaada wetu kwa familia ya mhasiriwa.
Afisa mkuu wa bustani hiyo bi Juliet Burgess amesikitishwa sana na tukio hilo.
''ni tukio la kuhuzunisha sana kupoteza maisha katika bustani hii''
''Hata hivyo ni mapema sana kuelezea nini kilichotokea hasa lakini uchunguzi wa kina unaendelea'' alisema Sajini Juliet Burgess
Mwanamke huyo alivamiwa na mnyama huyo alipokuwa ameingia kwenye eneo anakoishi ilikuisafisha kwa mujibu wa duru za habari nchini humo.
Bustani hiyo ya wanyama sasa imefungwa huku uchunguzi ukianzishwa kubaini kilichotokea.
Hadi sasa haijabainika iwapo bustani hiyo ambayo imefungwa kwa muda itachukua hatua zipi ima ni kumpiga risasi mnyama huyo ama l.
Hii si mara ya kwanza kwa wahudumu wa bustani ya wanyama kukumbwa na msiba kama huu.
Mwaka wa 2012 mwanamke mwengine aliuawa na tembo katika bustani ya Frankline kusini mwa Auckland nchini humo humo.
Monday, 21 September 2015
Chui amuua mhudumu New Zealand
Related Posts:
Wanajeshi washika doria mjini Bangkok..... Wanajeshi walinda baadhi ya ofisi za serikali mjini Bangkok Maelfu ya polisi pamoja na wanajeshi wamepelekwa katika mji mkuu wa Thailand Bangkok kwa jari… Read More
Unajua kinachoendelea kuhusu yule mwanamke wa Sudan aliyehukumiwa kunyongwa kutokana na kuolewa na mume mkristo...? Habari iliyoenea sana kwenye siku hizi za karibuni ni kuhusu mwanamke wa Sudan ambae amekua akisubiria hukumu ya kunyongwa kwa kosa la kuolewa na mume mkristo huku dini ya baba yake ikiwa inajulikana wazi kwamba ni… Read More
Serikali yamtuhumu Balozi wa Uingereza Serikali imetangaza rasmi mgogoro wa kidiplomasia kati yake na Balozi wa Uingereza nchini ikimtaka kujieleza kwa madai ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi. Mgogoro huo ulitangazwa bungeni mjini Dodoma jana… Read More
Makasisi waliotekwa nyara waachiliwa. Kituo cha uhamiaji kati ya mpaka wa Cameroon na Nigeria Makasisi wawili kutoka nchini Italy pamoja na mwanamke mmoja raia wa Canada walio… Read More
Rais mpya wa Malawi aingia rasmi madarakani leo Rais Mutharika akikagua gwaride katika uwanja wa Kamuzu Maelfu ya watu wamehudhuria sherehe za kukabidhiwa mamlaka kwa Rais mpya Peter Mutharika. Bwana Mu… Read More
0 comments:
Post a Comment