Facebook

Thursday 24 September 2015

TFF YAPIGA MARUFUKU ITIKADI ZA KISIASA KATIKA MECHI YA SIMBA NA YANGA

Shirikisho la soka nchini Tanzania limepiga marufuku kuvaa jezi ama mavazi yenye itikadi ya vyama vya siasa kwa mashabiki wanaotarajia kuona mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara baina ya Simba na Yanga Jumamosi Septemba 26 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini hii leo Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF Baraka Kizuguto amesema jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha amani inakuwepo kwenye mchezo huo, ambao unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu hizo zenye upinzani wa jadi Tanzania.

Wakati huo huo viingilio vya mchezo huo vimetangazwa leo ambapo kiingilio cha chini kitakuwa ni shilingi elfu saba (7,000).
Katika mchezo huo kiingilio cha juu kitakuwa ni shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa viti vya VIP A, Elfu Ishirini (20,000) kwa viti vya VIP B & C.

0 comments:

Post a Comment