Facebook

Saturday 19 September 2015

Wenger akataa kuzungumzia suala la yeye kushikana mkono na Mourinho.

Arsene Wenger leo amegoma kuweka wazi kama atapeana mkono na Jose Mourinho lakini ameweka kando juu ya umuhimu wa uhusiano wao kutokwenda vizuri kuelekea ziara ya Arsenal kwenda kuwatembelea Chelsea.

Mameneja hao wawili walionekana kukwepana mwishoni mwa mwezi August kwenye mpambano wa Ngao ya jamii uliofanyikia Wembley.

Walionekana pia kukwaruzana sambamba na matokeo ya ushindi wa goli 2-0 wa the Blues msimu uliopita- huku Wenger akimsukuma Mourinho walipozozana kufuatia Gary Cahill kumchezea vibaya Alexis Sanchez.

Akiulizwa na Standard Sport kama atapeana mkono na Mourinho kesho Stamford Bridge, Wenger amesema:”Sitaki kuzungumzia kuhusu jambo hili” akaongezea zaidi:”Sita ongea zaidi ya hichi nilichokwambia”
Mourinho ameacha mashambulizi yake juu ya Wenger kwenye wiki ya ufunguzi ya msimu lakini aliulizwa kama hayo maneno yana ukweli wowote, Mfaransa huyo alijibu: “hilo swali ungemuuliza yeye. Nina lenga juu ya kile ninachokipenda ambacho ni mpira. Ninamuheshimu kila mtu kazini na nina lenga juu ya ninachokipenda na sikingine ni mpira. Kusema kweli hayo mengine haya nihusu mimi zaidi.”
Mpambano kati ya Chelsea na Arsenal utapigwa kesho majira ya saa 8:45 mchana (Muda wa Afrika Mashariki). Nani atapigwa kesho?

0 comments:

Post a Comment