Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Marekani katika siku ya kwanza ya ziara ya kihistoria nchini humo ambapo amelakiwa na Rais wa nchi hiyo Barack Obama.
Papa Francis aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Andrew Air Force Base kutoka nchini Cuba.
Huku Marekani ikiwa na zaidi ya waumini wa Katoliki wapatao milioni sabini ziara hiyo ya papa inaoneka kuwa tukio kubwa nchini humo.
Kiongozi huyo wa kidini ambaye anaitembelea Marekani kwa mara ya kwanza atafanya ziara na kuongoza ibada katika miji ya Washington, New York na Philadelphia.
Wakati Papa Francis akiondoka nchini Cuba Papa Francis aliwaambia waandishi wa habari kuwa yeye sio muumini wa mlengo wa kushoto kama wengi wanavyodhani.
Papa alisema hatazungumzia suala la vikwazo vya biashara kati ya Cuba na Marekani, licha ya kuchukua nafasi muhimu katika mazungumzo ambayo yamesababisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili kurejeshwa mapema mwaka huu.
Wednesday, 23 September 2015
Papa awasili Marekani apokewa na Obama
Related Posts:
Uhalifu dhidi ya binadamu Sudan Kusini !! Viongozi wa Sudan Kusini wanatarajiwa kukutana kwa ajili ya kurejesha amani nchini humo Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu vita vy… Read More
19 wauwa katika mlipuko Nigeria.......... Waliojeruhiwa walikimbizwa hosipitalini Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa watu 19 wameuawa… Read More
Dunia yalilia wasichana Nigeria Maandamano dhidi ya serikali ya Nigeria kutaka wasichana waliotekwa nyara waokolewe Rais… Read More
Barclays kupunguza wafanyakazi elfu 19 Benki ya Barclays ya Uingereza imepanga kupunguza wafanyakazi 19,000 ifikapo mwaka 2016, kati yao elfu kumi wakiwa wafanyak… Read More
ANC kinaongoza kwa asilimia 60 Shughuli ya kuhesabu kura bado inaendelea Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress kinaongoza katika ucha… Read More
0 comments:
Post a Comment