Tanga. Kocha wa Simba, Dylan Kerr amefichua siri ambayo ni vigumu kuiamini.
Alisema alilazimika juzi kupanga viungo wengi dhidi ya Mgambo JKT kutokana na kupewa taarifa kuwa timu hiyo inacheza soka la kushambulia kwa wakati wote.
Hata hivyo, alisema alichokiona ndani ya dakika 20 za mwanzo wa mchezo huo kilikuwa ni tofauti.
Alisema baada ya dakika 20 alibaini kuwa taarifa alizopewa na kile kilichokuwa kikifanyika uwanjani haviendani, hivyo akaamua kumwingiza Hamis Kiiza ili achukue nafasi ya kiungo.
Simba, juzi iliingia uwanjani Mkwakwani na viungo wanne, Awadhi Juma, Justice Majabvi, Mwinyi Kazimoto na Said Ndemla na mshambuliaji mmoja, Mussa Hassan ‘Mgosi’ pekee mbele.
Kerr alisema kama siyo timu yake kufunga bao katika dakika ya 27 alipanga kumpa Kiiza nafasi ili kuongeza nguvu katika ushambuliaji, lakini alilazimika kufanya mabadiliko hayo wakati wa mapumziko kwa kumpunguza kiungo mmoja.
“Niliambiwa Mgambo wanacheza soka la kushambulia na kufunguka, hivyo nikaona ni vizuri nianze na viungo wengi, lakini hadi dakika ya 20 nilibaini kuwa hawako hivyo na kuona kama namchelewesha Kiiza uwanjani. “Yawezekana tungekuwa na matokeo mazuri zaidi kama Kiiza angeanza, lakini ilikuwa ni vizuri kuanza vile kwa kuwa sikuwahi kuwaona Mgambo,” alisema.
Hata hivyo, nahodha wa Mgambo, Fully Maganga alisema Simba iliwazidi katika kiungo na ndiyo sababu timu yao ilishindwa kucheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi kama ilivyokuwa katika michezo mingine waliyocheza dhidi yao.
“Timu yetu ilishindwa kucheza vizuri kwa kuwa Simba walijaza viungo wengi, tulipata shida kucheza nao katika eneo la kati, hivyo kuifanya timu yetu ionekane kuwa chini,” alisema Maganga.
Simba yanogewa Tanga
Katika hatua nyingine, baada ya kushinda mechi mbili jijini hapa, Simba imeamua kubaki huko ili kujiandaa na mechi yao ya Jumapili dhidi ya Kagera Sugar.
Kikosi hicho kiliendelea na mazoezi jijini Tanga na kitarejea Dar es Salaam leo na kupumzika Jumamosi kabla ya kuivaa Kagera Jumapili, ikiwa ni jitihada za kujiweka mbali na Yanga wanayokutana nayo Septemba 26.
Friday, 18 September 2015
Kerr : Kumbe Simba SC walinidanganya kuhusu Mgambo
Related Posts:
Kifungo cha kutosaini wachezaji:Barca wajipa moyo, wana imani wataruhusiwa......fuatilia hapa.... Barcelona ina imani kubwa kuwa wataweza kusaini Wachezaji wapya mwishoni mwa Msimu huu licha ya F… Read More
Simba,Yanga Matumbo Joto......kariakoo derby Jumamosi..... PAZIA la ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 linafungwa kesho aprili 19 kwa timu zote 14 kushuka uwanjani katika miji tofauti nchini. Ligi inamalizika kesho wakati timu tatu zimeshajihakikishia nafasi tatu… Read More
Barca Majanga....Alba na Neymar Nje wiki nne.......soma hapa.... Mshambuliaji wao raia wa Brazil, Neymar ataa nje ya uwanja wa wiki nne, wakati naye beki Jordi Alba atakaa muda kama huo baada ya wote kupata majeruhi. Klabu ya Barcelona imethibitisha kuwa Neymar alipata maj… Read More
Makombe feki ya kombe la dunia zaidi ya 1000 yakamatwa huko China....soma hapa.... Maofisa wa kuzuia bidhaa zisizo na hati miliki nchini China wamekamata makombe feki ya kombe la dunia zaidi ya 1,000 katika ghala ya kampuni moja kubwa ya utengenezaji na usafiris… Read More
Man Utd Wakubaliana dili na Sporting Lisbon Kusajili William Crvalho Manchester United imekubaliani Dili na Sporting Lisbon kumsaini Kiungo William Carvalho ambae pia huchezea Timu … Read More
0 comments:
Post a Comment