Facebook

Thursday 24 September 2015

NINACHOAMINI MAESTRO:MATARAJIO NA UHALISIA WA SEPTEMBER 26. SIMNA SC vs YANGA.

Na: Ayoub Hinjo(Ayo's Mata Maestro)  September 26 ni siku ambayo kila shabiki na mpenzi wa mpira hapa nchi ameiweka kwenye kichwa chake. Ni siku ambayo imejaa matarajio kuliko uhalisia wa tukio lenyewe. Ni siku ambayo Tanzania itasimama kwa dakika 90 kushuhudia nyasi za taifa zikiwaka moto. 

Matarajio ya wengi ni makubwa sana kuelekea kwenye mchezo huo. Kila upande unaamini wana timu bora kuliko upande mwingine. Kila upande unaamini kubeba ubingwa bila kumfunga mtani wako hakuna raha ya ubingwa huo. Miaka ya hivi karibuni matarajio yamekuwa yanateka hisia za wengi kuliko uhalisia wenyewe wa mchezo ambao umewekewa matarajio. Matarajio ya wengi ni kuona pambano lenye burudani,ufundi na raha lakini uhalisia unameza matarajio hayo wanayotarajia.  

Uhalisia wake ndio unatunyamazisha na kutukumbusha mpira ni dakika 90 na mpira ni mchezo ambao hauchezwi chumbani. Uhalisia wake ndio unatuonyesha mchezo ni wa kawaida sana ambao hauna ufundi wala burudani iliyotarajiwa.

Uhalisia wake unatuonyesha mchezo ni wakukamiana na butuabutua zisizokuwa na msingi. Maandalizi yanayofanywa kuelekea mchezo huo hayafanani kabisa na uhalisia unaokuja kuonekana uwanjani.  

Matarajio yetu sidhani kama yanaweza kuzidi uhalisia wake. Kama matarajio yatafanikiwa kutimia basi wote tuna haki ya kujaza viti 60000 ambavyo vipo uwanja wa taifa. Picha za mchezo huo tayari zimeshajengwa kwenye vichwa vya watu wengi,lakini picha hizo zitakuja kufutwa kwenye vichwa hivyo kutokana na uhalisia ambao utatokea uwanjani.  

Sitaki kumaliza yote,nahifadhi maneno yangu ili mwishowe nijue ni kipi kitakuwa kimefanikiwa kutimia siku hiyo kati ya matarajio au uhalisia wa Kariakoo derby. Hadi sasa matarajio ni mengi kuliko uhalisia halisi wa mchezo huo. September 26 kila kitu kitajulikana kama ni Matarajio yetu ni sahihi au siyo sahihi.

0 comments:

Post a Comment