Facebook

Sunday, 27 April 2014

D-Knob afunguka kwa nini aliamua kufunga ndoa kimya kimya..............

Screen Shot 2014-04-26 at 10.31.56 PM


Baada ya kuibuka upya na kutoa ngoma mpya inayo hit kwa sasa inayoitwa NISHIKE MKONO,D-Knob atoa sababu za kuamua kufunga ndoa ya kimya kimya mwaka 2009 huku idadi ya watu waliohudhuria pamoja na maharusi wenyewe ikiwa sio zaidi ya 10 kuanzia kanisani mpaka walikoelekea baada ya kutoka kanisani.

Ameongea na  na kusema ‘nilitaka kuifanya na mwenzangu nikamwambia tumekua wapenzi lakini sasa yahitaji tuwe ndani ya ndoa akasema twenzetu tukaongozana mpaka kanisani padri akasema hamuwezi kuoana nyie mnajua hata ndoa ni nini?kuna hatua’




 Screen Shot 2014-04-26 at 10.26.30 PM

‘Siyo kitu ambacho  tulitaka kufanya kama watu wengi wanavyofanya ile kukaa kuchangishana kwa sababu mimi rafiki zangu wa karibu wote walikua block nisingetaka kufunga ndoa halafu mwisho wa siku tuanze kununiana kuwa huyu hajachanga yule kachanga chapili nilitaka kufanya ili niendelee na maisha yangu kama mtu unapoamua kufanya birthday’

‘Wazazi walipata taarifa mwishoni kwa sababu hata mzee katika risala yake maana tulikaa kwenye meza moja baada ya ndoa mzee akasema mimi sijui nakupa zawadi gani maana umeniambia jana tu,kitu tulichofanikiwa ni gauni la mke wangu maana ni gauni la gharama nashukuru Mungu lilitupa stress mwanzo lakini liliwahi’

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata matukio mbalimbali ya wasnii kwa muda muafaka bila zengwe

0 comments:

Post a Comment