Facebook

Tuesday 17 March 2015

ARSENE WENGER NA VIVULI VYA KINA PIRES,HENRY,LJUMBERG,EDU. SABABU TANO KWANINI ARSENAL ANAWEZA KUPITA MBELE YA MONACO NA SABABU TANO KWANINI MONACO ANAWEZA KUPITA MBELE YA ARSENAL.


Mwaka 2014 tajiri namba moja kwa sasa duniani bwana Bill Gates kwenye Andiko lake la Can Asians Miracle happen in Africa? Alizungumzia kitu kimoja cha muhimu sana .Nchi za Africa kutembea kwa kutumia vivuli vya nchi za Asian ili viweze kufanikiwa na kuwa na mafanikio makubwa kama waliyopata nchi za Asia.

Kuna kipindi ambapo mimi Kiyumbi nilibahatika kushuhudia Kidogo Arsenal ya 2001iliyobeba EPL.Pia nilishuhudia kwa kiasi kikubwa Arsenal ya 2003 iliyobeba EPL pia.

Arsenal ya 2003 pamoja na kubeba EPL ila kuna kitu ilifanya cha Ajabu.Wakati dunia Ikishuhudia Obafemi Martinz Akiwauwa Arsenal nyumbani kwao Highbury.Moja kwa Moja Watu waliitoa Arsenal.Ila walisahau kuna mchezo mwingine november 2013 ulitakiwa uchezwe san siro nyumbani kwao Intermilan.

Tulishuhudia Arsenal ikigeuza Magoli 3-0 kwa kuifunga goli 1-5 Intermilan nyumbani kwao.Kwa magoli ya kina Henry aliyefunga mawili, Ljumberg,Pires na Edu.

Leo hii ni miaka 12 tangia tukio hili litokee .Arsene Wenger Anatakiwa tena kupanda mlima mrefu wa Monaco.

Kama alivyosema Bill Gates mwaka jana kwa nchi za Africa kufanikiwa Wanahitaji kutembea kwenye vivuli vya nchi za Asia.Na leo hii kwa Arsenal kupindua matokeo wanatakiwa watembelee vivuli vya kina Pires,Henry,ljumberg,Edu na timu nzima ya Arsenal ya 2003.

Ni miaka mingi imepita tangia Ajax wapindue matokeo ya 3-1 waliyofungwa kwao na kumfunga Benfica 4-0 kwenye mechi ya marudiano.

Jiulize ,Ni Arsenal au Monaco ?

SABABU TANO KWANINI ARSENAL ATAPINDUA MATOKEO YA LEO.

1:Mipango ya Monaco kwenye mechi ya leo.Mimi kama Kiyumbi najaribu kujiuliza vitu vitatu.Cha kwanza Monaco atawaachia Arsenal wacheze ili yeye alinde magoli yake? Au Monaco Atashambulia ili aongeze faida ya magoli?  Au Monaco atacheza balance game afu autanue uwanja awapige Arsenal kwa counter attacks? Kama Monaco ataingia kwa mbinu mojawapo kati ya hzo naamn atapigwa.Hzi tunaziita mbinu za kujijenga zaidi.Na mechi kama hizi huhitaji mbinu kama hizi unahitaji mbinu za kumuuwa wenger zaidi na siyo mbinu za kujijenga.Ukimuuwa wenger umeiua Arsenal.Hili kosa walifanya Chelsea .Walishindwa kumuua blanc wakawa wanajijenga.Naamn kosa kama hili litatokeo leo.

2:Arsenal hajapoteza mechi yoyote tangia atoke kucheza na Monaco.Ameshinda dhidi ya QPR,Man united,Westham,Everton hii inawajengea hali kubwa ya kujiamini kwa Arsenal.

3:Kurudi kwa Ramsey na viwango vya wachezaji wa Arsenal.Ikumbukwe Arsenal ndo timu pekee yenye wafungaji wengi.Ina wafungaji 21 hii inaonesha timu haimtegemii mtu mmoja kwenye suala la Ufungaji.Pia ulejeo wa Ramsey ni chachu nzuri kwa Arsenal kwa sababu mechi kama hii inahitaji wapiganaji.Ramsey ni moja ya wapiganaji wazuri sana.

4:Arsenal msimu huu imeshinda mechi zote za ugenini za champion league.Wameshinda dhid ya Anderlech, Borrusia Dortmund,Galataslay.Hii inaonesha ni wazuri zaidi msimu huu kwa mechi za ugenini zaidi wakiwa Emirates.

5: Matokeo ya Hivi karibuni zidi ya Bayern munich.Wote tunajua Bayern ya kipindi cha karibuni ni nzuri zaidi ya Monaco hii.Arsenal iliweza kumfunga bayern 2-0 na msimu uliopita walidraw.Nguvu hizi wakiwekeza kwa Monaco kuna uwezekano Arsenal kumtoa monaco.

SABABU TANO KWANINI MONACO ATAMTOA ARSENAL.

Tangia tajiri Dimitry Rybolovlew aichukue monaco mikakati yake ni kuitengeneza monaco ya ushindani.Ndo Mana alinunua wachezaji wa majina makubwa.

Kwanini Monaco atapita leo?
1:Mpaka sasa Monaco kwenye uwanja wao wa nyumbani msimu huu wamefungwa magoli 7 tu.Tena kwenye mechi 4.Hii inaonesha ni wagumu sana kuruhusu magoli.Na ndo kinga yao leo ya kutofungwa magoli mengi leo.

2:Monaco mpaka sasa hivi kwenye uwanja wao wa nyumbani kwenye mechi 7 zilizopita zote hawajafungwa goli lolote.Yan wana clean sheet 7 mfululizo kwenye uwanja wao wa nyumbani mpaka sahivi.

3:Monaco mpaka sahv hawajafungwa mchezo wowote kwenye michezo 16 iliyopita ya mashindano yote.

4:Monaco wana njaa ya kuingia Robo fainali kwa mara ya kwanza baada ya miaka 5 .Hii itakuwa fursa yao kubwa kuingia Robo fainali ya UEFA baada ya miaka 5.

5:Faida ya magoli.Naamn kocha Leonard Jardim atakuwa amewaambia wachezaji wasibweteke na hadhina ya magoli waliyonayo.Ila kimchezo Hadhina waliyonayo ya magoli ni silaha tosha ya wao kujiamn na kufuzu mechi ya leo.

Nimemaliza shukrani kwa kusoma

Imeandaliwa na…………
                                        #Martin kiyumbi.

0 comments:

Post a Comment