Facebook

Sunday 22 March 2015

UCHAMBUZI WA MECHI KALI ZA LEO LIGI KUU UINGEREZA NA Mr CHOI (KWA TAARIFA YAKO)

LIVERPOOL vs MAN UTD
   Licha ya timu zote kutokuwa katika mbio za ubingwa huku mbio zao zikiwa kuwania nafasi ya nne ili kucheza kombe la mabingwa Ulaya bado historia inafanya mchezo huu kuwa na mvuto wa kipekee.

   Utawala wa Liver kwenye miaka ya 1975/90  huku wakichukua vikombe vya ligi kuu 18 ulivunjwa na Man Utd ambao waliibuka miaka ya 1993/13 kwenye kuchukua vikombe vya ligi na mpaka sasa wana vikombe 20.
   Ni sehemu moja tu ambayo bado Liver wanatawala kwa wingi wa vikombe napo ni ktk Uefa wakiwa wamechukua mara 5 huku Man Utd wakinyakua mara 3. Katika makabati ya timu zote Man Utd bado ni kinara wa vikombe wakiwa na idadi ya vikombe 55 dhidi ya 48 vya Liverpool.
   Ushindi wa Liverpool leo utakuwa wa 58 mbele ya Utd walioshinda mara 68 huku wakitafuta ushindi wa 69 na timu hizi zimetoka sare mara 44.
     Liverpool wapo nafasi tano wakiwa na pointi 54 wamekuwa na matokeo mazuri kwa kipindi cha hivi karibuni na endapo watashinda leo watafikisha michezo 14 pasipo kupoteza. Gerrard amekuwa na mchezo mzuri pindi akikutana na Man Utd huku akifunga mara 7 kati ya 11 kwenye mechi za Ligi.
    Henderson ambaye ameonekana kuvaa viatu vya Gerrard vyema atakuwa katika safu ya kiungo pamoja na Allen kupambana na Herrera pamoja na Carrick kama Van Gaal atamchezesha kati. Kwa ujumla vikosi vyote havita kuwa tofauti sana kutoka michezo waliocheza hivi karibuni.
   Licha kucheza vibaya kwenye mchezo wa awamu ya kwanza na kufungwa goli 3 Mignolet kwa sasa yupo ktk ubora mzuri akichagizwa na safu yake ya ulinzi inayocheza vyema.
    Man Utd wao wapo nafasi ya nne kwa pointi 56 ni timu pekee iliopata ushindi mara nyingi pale Anfield kuliko timu nyingine za ligi kwa hivi karibuni wanamichezo migumu hivyo mahesabu yalianza kwa Spurs na wanahitaji muendelezo wake licha ya kutokuwa wazuri hasa safu ya ulinzi ambapo De Gea amekuwa akifanya kazi ya ziada hivi sasa tangu Rooney arejeshwe kwenye nafasi yake ya ushambuliaji ameonesha nini hasa Man Utd wanastaili fanya na hii leo ata tafuta goli la 170 katika ligi.
   Mwamuzi wa mchezo huu ni Martin Aikison alie chezesha michezo 24 mpaka sasa huku akitoa kadi za njano 96 na nyekundu 5 na kwa aina ya ushindani uliopo wa timu hizi pengine atafikisha kadi 100 kwenye mchezo wake wa 25.

--------- 
HULL vs CHELSEA
     Ushindi wa Man City na Arsenal siku ya jana utawalazimu Chelsea kuibuka na ushindi leo ili kujipa matumaini makubwa ya kuchuku ubingwa wa ligi.
   Ukitizama mchezo wa Soton wiki iliopita walicheza vyema hasa kipindi cha pili mara baada ya kuingia Ramires ambapo Matic hakuwa vyema kwenye mchezo huo, mchezo wa leo kikosi ni kilekile hakito badilika labda upande wa golini na kuanza kwa Willian badala ya Oscar.
   Hull City wao watajaribu kuwa simamisha Chelsea ambapo wanatakiwa kuongeza gepu la pointi kati yao na timu zilizo mkiani mwa ligi. Hawana matokeo mazuri mbele ya Chelsea kwani katika michezo 11 ya karibuni wamefungwa mara 9 na kutoa sare 2.
   Kiungo Huddlestone hatokuwepo kutokana na kadi nyekundu aliopata kwenye mchezo wa Leicester pia Jelaviç atakosa mchezo huu kutokana na majeraha yatakayo muweka nnje wiki 6
   Hull wazuri kujilinda na mara nyingi Bruce amekuwa hafunguki sana pindi akicheza na timu kubwa huku timu yake ikishika nafasi ya pili kwa wingi wa kadi nyekundu ( 5 ) wakiongozwa na Aston Villa (6) . Mchezo utakuwa wa upande mmoja lakini tutaraji mashambulizi ya kustukiza kwa Hull watakao ongozwa na N'doye.

NB:  Hazard ametengeneza nafasi 79 kati ya 74 za Fabregas za kufunga.
  
For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com

0 comments:

Post a Comment