Facebook

Saturday 14 March 2015

Chamberlain nje wiki nne.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger atalazimika kujikuna kichwa baada
ya kupata habari kuwa kiungo chake cha kutegemewa Alex Oxlade-
Chamberlainhatakuwepo kwa takriban majuma tatu hadi nne zijazo
kutokana na jeraha nyuma ya goti.

Kulingana na kocha huyo,Chamberlain alipata jeraha hilo katika
mechi ya kukata na shoka ya FA dhidi ya wapinzani wao wa jadi
Manchester United jumatatu iliyopita.

Kujeruhiwa kwake ni pigo kwa azimio la Arsenal kuimarisha matokeo
yao katika ligi kuu ya Uingereza ambapo sasa wanashikilia nafasi ya
tatu .

Alex Oxlade-Chamberlain alichangia pakubwa katika ushindi wa 2-1
dhidi ya Manchester united katika FA
Aidha Arsenal wanajiandaa kwa mechi ya marudio ya mkondo wa 16
bora katika ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya ambapo wameratibiwa
kuchuana dhidi ya Monaco juma lijalo.

Winga huyo alikuwa amerejea mwishoni mwa mwezi Februari baada ya
kukaa mwezi mmoja nje kufuata jeraha lengine la kiuno.
Wenger hata hivyo alipata afueni katika safu ya ulinzi baada ya
kurejea kwa Gabriel aliyejeruhiwa katika mechi ngumu dhidi ya QPR
mnamo Machi tarehe 4.

0 comments:

Post a Comment