Facebook

Saturday 21 March 2015

Uchambuzi wa Mechi kali za leo ligi kuu Uingereza na Mr.CHOI (KWA TAARIFA YAKO).


     N'CASTLE vs ARSENAL
   Baada ya kutolewa Uefa huku akikosa kikombe cha FA,Capital one kocha wa Man City atajiuliza juu ya hatma yake pale Etihad endapo na ubingwa wa Ligi atashindwa kuchukua.
  Ni miongoni mwa walimu wazuri lakini asie na mbinu mbadala pindi akizidiwa kimchezo ukubwa wa kikosi chake na aina ya matokeo wanayopata ni vitu viwili tofauti.
  Leo kucheza na W.brom ilio chini ya Tony Pulis ambayo tangu aichukue imekuwa na matokeo mazuri yakichagizwa na safu yake ya ulinzi.
  Kuelekea mchezo wa leo City watamkosa Toure na Milner hivyo dimba la kati tutaraji kuwaona Fernando na Fernandinho na pembeni Silva pamoja na Nasri safu ya ushambuliaji itaongozwa na Aguero alie na rekodi nzuri mbele ya W.brom kwani kafunga mara nne kati ya tano ktk ligi dhidi ya W.Brom. Bonny anaweza pata nafasi ya kuanza mchezo wa leo kwani tangu atue City ajapata nafasi ya kuanza.
   W.Brom golini atakuwepo Myhill kutokana na majeraha ya Foster pia wata mkosa Brunt na Yacob achilia mbali majeruhi wa kipindi kirefu. Ni timu inayocheza kwa tahadhari sana huku wakishambulia kwa kustukiza kwa kumtumia Berahino alie ktk kiwango bora. Kwa kutizama matokeo ya hivi karibuni licha ya City kuwa na takwimu nzuri mbele ya W.Brom sare inaweza jitokeza kama City hawatabadilika.
  
NB: Katika michezo 10 City wameshinda mara 9 na kutoa sare 1.
    Michezo 12 ya hivi karibuni Etihad City wamepoteza mara 1 sare 3 na kushinda mara 8.

-------
   

     MAN CITY vs W.BROM
     John Corver amekuwa na matokeo mabaya tangu aichukue N'castle huku akipoteza michezo mitatu kati ya minne ya hivi karibuni. Ni miongoni mwa vikosi vilivyo na majeruhi wengi mpaka sasa huku pia ktk mchezo wa leo wakiendelea kumkosa mshambuliaji wao Cisse alie fungiwa kutokana na tukio la Evance kwenye mchezo dhidi ya Man Utd pia Coloccini alie onyeshwa kadi nyekundu kwenye mechi ya Everton.
     Kikosi hakita kuwa na mabadiliko sana kama kilicho cheza na Everton kwani  kati atasimama Colback na Sissoko huku Ameobi na Perez wakitokea pembeni Cabella atakuwa nyuma ya Riviere.
   Mzee Wenger upande wake licha ya kutolewa Uefa lakini bado kikosi chake kimekuwa na mchezo mzuri na matokeo mazuri kwa hivi sasa huku wakinyatia nafasi ya pili na ikibidi ubingwa.
   Coquelin amekuwa na kiwango bora kabisa ktk dimba la chini akisaidiana na Cazorla na Ramsey huku Ozil,Sanchez wakitokea pembeni Giroud anataraji kuongoza mashambulizi na amekuwa na takwimu nzuri dhidi ya Magpies kwani kasha funga mara sita kati ya tano alizo cheza nazo.
   Umakini hasa utakuwa kwa Sissoko ambaye amekuwa mzuri sana katika kuanzisha na  kulazimisha mashambulizi kwa upande wa Magpies.
  Kwenye michezo nane Arsenal hawajapoteza mbele ya N'Castle ni timu tofauti kwa hivi sasa Arsenal wakiwa katika kiwango bora dhidi ya Magpies wanao jaribu kutafuta matokeo mazuri, mchezo utakuwa wa kufunguka sana kulingana na uchezaji wa timu zote na umakini utahitajika kwa safu ya ulinzi ya N'castle.


For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com

0 comments:

Post a Comment