Facebook

Saturday 21 March 2015

Kenya:Binti wa miaka kumi(10) ajifungua mtoto wa kiume

GLADYS CHELAGAT.AKIWA NA MTOTO WAKE.
Wakati wanaharakati mbali mbali duniani wakipambana kupinga ukatili kwa watoto, huko nchini Kenya mtoto wa miaka 10 ambaye angetakiwa kuwa shuleni akisoma na kucheza na wenzake michezo mbali mbali, anapata jukumu la kumlea mtoto mwenzake. 

Gladys chelagat, anakuwa mama mdogo kabisa duniani baada ya kujifungua mtoto wa kiume jumamosi iliyopita akiwa na umri wa miaka kumi tu (10).

Mtoto huyu alijifungua mtoto wake wa kiume mwenye uzito wa kg 2.8 katika hospital ya kericho nchini kenya.

Hata hivyo Mungu ni mkubwa  kwani pamoja na udogo wa mtoto huyu alijifungua salama bila ya kupata tatizo lolote la kiafya.

0 comments:

Post a Comment