Facebook

Saturday 14 March 2015

Watumia mifuko ya plastiki badala ya kondomu Uganda.

Mahitaji yanafanya waganda kuwa wabunifu hata katika masuala ya
kondomu.
Katika eneo la Kiyindi, wilaya ya Buikwe-mashariki ya Kampala, watu
wanatumia kondomu bandia –wao huita “buveera- kutokana na
mifuko ya plastiki.

Wenyeji wa Kiyindi wanadai ama kondomu ni ghali au hakuna kabisa.
Siraj Kalyango alifika huko kujionea kwa macho yake na aliporejea
Kampala ametutumia taarifa ifuatayo.
Uganda inahitaji mipira ya kondomu million 20 kila mwezi hii ni kwa
mujibu wa wizara ya afya na tume ya Ukimwi takwimu za mwaka
2013.
Hata hivyo kondomu hizo hazitoshi na mahali zipo bei yake ni ghali
mno haswa kwa taifa ambayo asilimia kubwa ya watu wanaishi kwa
kipato cha chini ya dola moja kwa siku.
''Hapa kwetu kweli kuna ukosefu mkubwa sana wa mipira ya
kondomu ,imezidi matarajio ya wengi na hivyo inawalazimu watu
kustarehe mwili kwa mwili na unajua tena hiyo ni hatari sana
maanake
waweza kuambukizwa magonjwa mengi na tena yale ambayo hayana
tiba''anasema mkaazi wa kiyingi.

''Wakati mwengine ukiwa nayo unaitumia lakini je ukikosa ?''
Mifuko ya plastiki inatumika kwa wingi miongoni mwa jamii ya
wavuvi
Hawa ni baadhi tu ya wenyeji wa mji wa Kiyindi iliyoko karibu na
ufukwe wa ziwa Victoria katika wilaya ya Buyukwe nchini Uganda.
Mwanasosholojia , Derick Motema ambae alikwenda Kiyingi miezi
michache iliiambia BBC yaliyomfika.

''Mwanamke mmoja alinivuta na kuiniingiza ndani ya chumba chake
akataka kufanya kitendo cha ngono kwa malipo, nikamuuliza iwapo
anamipira ya Kondomu akasema hana lakini akasema kuwa
alikuwa na karatasi za plastiki ambayo tungeifunga kwa mipira ya
elastiki (bladder) alisema Motema
''Tulikuja hapa Kihindi miezi miwili iliyopita kuhudhuria kongamano la
kimatibabu iliyoandaliwa na mbunge wa eneo hili .
Nilikuwa naongoza kundi ambalo lilikuwa linanyunyuzia dawa ya
kuuwa wadudu kama vile kunguni ndani mwa nyumba za wakazi huko.

Katika pitapita yangu nikafika kwenye danguro ambako kulikuwa na
makahaba wengi.
Waliponiona wakanijia wakidhani kuwa mie ni mteja na mmoja wao
akanivuta hadi ndani ya chumba chake.
Ndani huko akaniomba hela ili tufanye kitendo cha ngono.
Uhaba wa Kondomu unatokana ukosefu wa wahisani
Mie nikamwambia kuwa sikuja kufanya hilo ,lakini yeye
akang'ang'ania kufunga lango.

Sasa nikawambia ikiwa anataka tufanye kitendo hicho nikataka kujua
ikiwa walikuwa na mipira ya kondomu na nilitaka kuinona.
Akaniambia hana mipra ya kondomu lakini akapendekeza kuwa
wanakondomu mbadala ya mpira wa plastiki naweza kuivaa na
nikaifunga mipira ya raba.
Mambo hayo yalinigusa sana kwani nilifikir kuwa kuna baadhi ya
wanaume ambao wanatumia hizo kondomu mbadala.

''Ukweli ni kwamba wanawake makahaba wapo hapa chungu nzima
anasema mkahazi mwengine wa eneo hilo Omari Ejaga.
Kiyindi ni kituo cha biashara ambacho kinapatikana kandokando mwa
Ziwa Victoria katika wilaya ya Buikwe umbali wa kilomit 120-
mashariki mwa jiji kuu la Kampala.
Kina watu wengi kutoka sehemu tofauti za nchi pamoja na je yake
ambao wengi wanajihusisha na uvuvi il hali wengine na biashara
mbalimbali.
Nilifika mahali pa danguro alilotaja Bw Motema kutaka kujua ukweli
ikwa wanatumia mifuko ya plastiki badala ya kondomu, lakini juhudi
zangu ziliambila patupu akina mama hao walipogundua kuwa mimi ni
mwandishi habari .
Bi Annet Nabasinda ni mfanya biashara ya kuuza vifaa vya
kuwarembesha wanawake .

Wanaume wengi hawataki kutumia mipira ya Kondomu wakidai
inawapunguzia hisia
Nilimuuliza mtazamo wake iwapo matumizi ya mipira ya kondomu ni
makubwa Kiyingi ,lakini akakanusha .
Annet anasema kuwa katika mtaa huo si ajabu kumuona mwanamke
ambaye anajulikana wazi kuwa ni mgonjwa lakini wampata ana
mimba.

Mfanyakazi wa kituo cha afya cha jamii Makonge –Kiyindi Justin
asema kuwa kiwango cha kuenea kwa UKIMWI na magonjwa mengine
ya zinaa katika wilaya ya Buikwe ni kubwa mno.
Anasema kuwa kondomu hazitoshi kwa sababu yamkini wahisani
wamepunguza usambazaji wake kufuatia mtafarauku na serikali
kufuatia kupitishwa kwa sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Aidha anasema kuwa japo watu wana hela lakini hawataki kununulia
mipira ya kondomu bali huamua kununua vitu vingine vya dharura
kama vile chakula na mahitaji mengine ya kila siku.
Buikwe inakuwa ya nne kwa idadi ya maambukizi kwa kuwa jamii
kubwa inajihusisha na biashara ya samaki usambazaji ni mkubwa.

''Sina takwimu ninazoweza kulinganisha lakini kasi ni kubwa kuliko ya
taifa ya 7.5 au 7.6 anasema.
''Kwa hivyo ikiwa kuna msamaria mwema anaeweza kuleta kondomu
na kuzigawa kwa jamii litakuwa jambo jema kwani kuna mahakaba
wengi hapa'
lakini tunamshukuru Mungu kuwa wako hiari kupimwa Ukimwi
ukiwafikia''.

Wanawake wa jamii hiyo wanadai hawawezi kuishi bila ya ngono
japo waume wao wamekwisha aaga kutokana na ukimwi
Hata hivyo afisa wa chama cha msalaba mwekundu Kiyindi yeye
anasema akuwa kondomu zipo za kutosha ila watu ndio hawataki
kuzichukuwa.

Ameongeza kuwa wengine wanaona haya kuuliza kondomu madukani
na hata katika zahanati za afya.
Kauli yake inapingwa na baadhi wakitoa sababu ambazo Bi Anne
Nabasinda amezisikia.
''Wanaume wengi wanasikika wakiwauliza hawa machangudoa iwapo
wamewataka hao inakuwaje wanawataka watumie mipira ya Kondomu
ama plastiki''
''Wengine wanadai kuwa wazungu wameweka vitusi vya ukimwi katika
mipira ya kondomu iliwapunguze idadi ya Afrika'' anasema Annet
Nabasinda .

Ama kweli mahitaji yanamlazimisha mwanadamu kujikuna kichwa lakini
hatua wakazi wa Kiyindi Biukwe kutumia 'karatasi za plastiki za
mkate -buveera'' kama kondomu mbadala si jambo la kuigwa.

0 comments:

Post a Comment