Facebook

Tuesday 3 March 2015

Mtuhumiwa namba moja kwa utapeli wa viwanja akamatwa Dare es salaam

"MTUHUMIWA SUGU UTAPELI WA VIWANJA DAR MBARONI

Mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa kinara wa utapeli wa viwanja jijini Dar es Salaam (jina linahifadhiwa kwa sasa), leo anatarajiwa kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, kujibu tuhuma zinazomkabili.
 
Mtuhumiwa huyo ambaye aliwahi kufanyakazi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anadaiwa kutapeli zaidi ya viwanja 30, kikiwamo cha familia ya Mwalimu Julius Nyerere na cha Katibu Mkuu wa Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, pamoja na cha mwanamke mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi Umoja wa Mataifa (UN). Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo."

Mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa kinara wa utapeli wa viwanja jijini Dar es Salaam (jina linahifadhiwa kwa sasa), leo anatarajiwa kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, kujibu tuhuma zinazomkabili.

Mtuhumiwa huyo ambaye aliwahi kufanyakazi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anadaiwa kutapeli zaidi ya viwanja 30, kikiwamo cha familia ya Mwalimu Julius Nyerere na cha Katibu Mkuu wa Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, pamoja na cha mwanamke mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi Umoja wa Mataifa (UN). Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

0 comments:

Post a Comment