Facebook

Friday 20 March 2015

Yaya Toure na nyota wengine wafunguliwa milango ya kuondoka Man City.

Mabingwa wa ligi ya Uingereza Manchester City watamuuza Yaya
Toure msimu huu katika mpango unaolenga kuwauza wachezaji
wengine wa kilabu hiyo kwa lengo la kununua wachezaji chipukizi
watakaoongozwa na mchezaji Kevin De Bruyn wa Wolfsburg.

Kushindwa kwa kilabu hiyo na Barcelona katika mechi ya kufuzu kwa
robo fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya kumethibitisha kwamba
mabadiliko makubwa yanahitajika katika kilabu hiyo.

Katika wachezaji kumi na moja walioanzishwa katika mechi dhidi ya
Barcelona ni Sergio Aguerro mwenye umri wa maka 26 aliye chini ya
umri wa miaka 27.

Huku Aguerro,Joe Hart,Vincet Kompany,Fernandinho na David Silva
wakiwa na maisha marefu katika kilabu hiyo ,waliosalia huenda wakauzwa.

Hii inamaanisha kwamba Yaya Toure,Bacary Sagna,Martin
Demichelis,Alkesandar Kolarov ,Samir Nasri na James Milner ambaye
kandarasi yake inaisha hatma yao haijulikani.

Kati ya wachezaji ambao hawakuanzishwa katika uwanja wa Nou
Camp siku ya jumatano usiku,Gale Clichy,Pablo Zabaleta,Jesus
Navas,Fernandinho,Steven Jovetic na Edin Dzeko huenda pia
wakauzwa.

Frank lampard amesema kuwa anaondoka ili kujiunga na kilabu ya
New York City nchini Marekani.

0 comments:

Post a Comment