Facebook

Wednesday 11 March 2015

UCHAMBUZI WA MECHI ZA LEO LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA NA Mr.CHOI

      CHELSEA ¹ vs ¹PSG
  B.MUNICH 0 vs 0 S.DONESK.
                    22:45

   Msimu uliopita ktk dimba la
  Parc des Princes Jijini Paris Chelsea walifungwa 3-1 na mchezo wa marudiano pale darajani Chelsea walishinda 2-0 huku Demba Ba akiwa shujaa wa mchezo huo baada ya kufunga goli la dakika za mwisho na kuipeleka Chelsea katika hatua inayofuata kwa faida ya goli la ugenini walilo lipata pale Parc des Princes.
     Mambo yamekuwa tofauti msimu huu kwani mchezo wa awamu ya kwanza pale Paris  timu hizi zilitoka sare 1-1 kwa magoli ya Ivanovic kwa Chelsea na Cavani upande wa Psg hivyo kupelekea mchezo kuwa mgumu siku ya leo kwani Chelsea wataitaji sare ya bila kufungana au ushindi wapinzani wao watahitaji ushindi au sare ya magoli zaidi ya moja.
    Hakuta kuwa na mabadiliko makubwa kwa timu zote tutaraji vikosi vilevile vilivyocheza mchezo wa awamu ya kwanza huku David Luiz akirejea Darajani baada ya kuuzwa msimu uliopita.
     Endapo Psg watafunguka zaidi kama ilivyokuwa kipindi cha pili ktk mchezo wa awamu ya kwanza kwa kuwatumia mabeki wake wa pembeni kwa ajili kupiga krosi itawapa Chelsea tabu hasa kutokana na umahiri wa Cavani na Ibrahimovic kwenye mipira ya juu.
     Chelsea mara nyingi wamekuwa wazuri kwenye mipira iliokufa huku wakichagizwa na  Hazard ambae mpaka sasa ndie mchezaji aliyechezewa faulo nyingi ktk msimu huu wa Uefa 28 na kati ya hizo 9 ni mchezo wa awamu ya kwanza dhidi ya Psg, watahitaji kushambulia zaidi huku wakijilinda kutokuruhusu goli kwani matokeo yakiwa 0-0 ni faida kwao hivyo umakini hasa kwa Cavani na Ibrahimovic unahitajika.
   Vita kubwa itakuwa katika safu ya kiungo kwa timu zote kutokana na umahiri mkubwa wa viungo wa timu hizo Matuidi,Luiz,Ramires na Matic anae tarajiwa rejea ktk kikosi cha Chelsea.
   Tangu goli la Fernando Morientes alipo kuwa Monaco kwenye nusu fainal 2003/04 Darajani pamekuwa pagumu kwa timu kutoka Ligue¹

NB:: Chelsea na Fc Porto ndo timu pekee mpaka sasa hazija fungwa ktk michuano hii ya Uefa msimu huu.
 
-----------------------------------------------

         ALIANZ ARENA:-

     Vinara wa Bundesliga Bayern Munich watawakabili vijana wa Mircea Lucescu Shaktar Donesk.
   Katika mchezo wa awamu ya kwanza tulishuhudia sare ya 0-0 huku Xabi Alonso akilimwa kadi nyekundu hivyo hatokuwepo katika mchezo wa leo.
   Safu ya ulinzi ya Donesk ilicheza vyema sana kwenye mchezo wa awamu ya kwanza hasa ukilinganisha na safu ya ushambuliaji ya B.munich iliyo bora kabisa, Fernando na Fred watakuwa na kazi ya kufanya dhidi ya kina Schweinsteiger kwani hawana historia nzuri ugenini dhidi ya timu za Ujerumani .
   Umakini hasa utahitajika hasa kwa Bayern kutokana na staili ya uchezaji ya Shaktar hasa wanavyo mtumia Douglas Costa, Teixeira na mshambuliaji anaeongoza kwa magoli mpaka sasa Adriano(9) hasa kwa mashambulizi ya kushtukiza
   Bayern watahitaji ushindi huku wapinzani wao wakihitaji sare ya magoli au ushindi.
   Martínez,Lahm,Alcàntara na Alonso  hawatacheza mchezo wa leo kwa upande wa Bayern na wapinzani wao Bernard hatokuwepo huku Ordets , Kryvtsov wakiwa hawana uhakika.
    Vyacheslov,Rakitsky, Oleksand na Sirna wanatakiwa kuwa watulivu na makini hasa kwa Robben ambae anauwezo wa kubadili matokeo mda wowote. Mtanange utakuwa mgumu kulingana na aina ya matokeo ingawa historia inawabeba Bayern.

For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com

0 comments:

Post a Comment