Facebook

Thursday 26 March 2015

Rais afanya uteuzi wa Wabunge wapya.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wabunge wawili (2) wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Walioteuliwa ni Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba.

Rais amefanya uteuzi huu kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e) ambapo amepewa mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi 10.

Uteuzi huu umekamilisha idadi ya wabunge ambao Mheshimiwa Rais amepewa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kikatiba.

Wabunge ambao wameshateuliwa ni:

Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
Mhe. Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo
Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro
Mhe. Janet Zebedayo Mbene
Mhe. Saada Salum Mkuya
Mhe. Zakhia Hamdani Meghji
Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
Mhe. James Fransis Mbatia

Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Machi, 2015.

Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu-Dar-Es-Salaam

0 comments:

Post a Comment