Facebook

Saturday 21 March 2015

Hivi ndivyo Van Gaal alivyoiandaa Man United kuwakabili Liverpool.

Lous Van Gaal aeleze jinsi alivyo isuka timu ya Manchester United
kwa ajili ya mchezo wa jumapili dhidi ya Liverpool
kocha huyo mwenye asili ya kiholanzi alitoa maelekezo na mpangilio
mzima wa maandalizi ya timu yake ambayo itavaana na Liverpool
mapema mwishoni mwa wiki hii.akiongea na gazeti la The Daily
Telegraph Van Gaal alisema

"Maandalizi yana anzia na maskauti,Paul Brand,ambae
anawachunguza wapinzani wetu,ambae ana chagua picha zote na
Marcel Bout ambae ni skauti wa timu pinzani
Marcel Bout mara kwa mara huwa anakwenda kutazama mechi za
wapinzani wetu wiki mbili kabla ya mechi nao,kwa sababu baada ya hapo tutakutana nao nyumbani au ugenini.
"Pia Ryan Giggs ana andaa takwimu zilizo kusanywa na Marcel Bout
pamoja na Paul Brand kwa ajili ya kuwaonyesha wachezaji"

"baada ya hapo tuna andaa mpango wa mechi kwa sababu ya
uchambuzi,tunajadili mpango wa mechi"
"siku inayo fata tuna wasilisha kwa wachezaji.Giggs ndio huwa
anafanya hivyo,hivyo hufanya mkutano mwingine na wachezaji
wanatakiwa watazame,sisi tuna waelezea,baada ya hapo tunakwenda
na kufanyia mazoezi mpango wa mechi ,wachezaji 11 dhidi ya
11.Ryan Giggs anafundisha timu pinzani aliyo ichambua.

"Albert Stuivenberg anafundisha timu yangu.baada ya hapo
tunafanya mazoezi kupitia njia tofauti tofauti.tuna rekodi vipindi
vya mazoezi.

"mkutano unao fata ni mkutano wakuunganika,tunafanya na
mabeki,viungo na washambuliaji'

'Albert anakuwa amekusanya muonekano mzima wa mazoezi lakini pia
na mechi zilizo pita ambao uanaeleza zaidi mpango wetu wa mchezo"

0 comments:

Post a Comment