Facebook

Friday 20 March 2015

Makao Makuu ya Rais yashambuliwa Yemen

Rais wa Yemeni Abd Rabbuh Mansour Hadi amehamishwa hadi mahala
salama baada ya mashambulio ya angani katika maskani yake katika
mji wa Aden, Kusini mwa taifa hilo.

Bwana hadi alitoroka kutoka mji wa Sanaa ambao umetekwa na
Waasi wa Houthi na anajaribu kujenga kambi mpya ya utawala katika
eneo hilo.

Ndege mbili za kivita zinaaminika kutumika katika mashambulio hayo,
lakini maskani yake hayakushambuliwa moja kwa moja.
Ndege hizo zinadaiwa kutumwa kutoka mji wa Sanaa.

Uvamizi huo ulitokea saa chache baada ya jeshi la Hadi kutibua
shambulizi katika uwanja wa ndege wa kimataifa lililotekelezwa na
vikosi vitiifu vya Houthi.

0 comments:

Post a Comment