Facebook

Saturday 21 March 2015

Van Gaal atumia mazoezi ya kukera kuwandaa wachezaji wake dhidi ya Liverpool.

Kocha wa Manchester United,Lous Van Gaal amekua kama refari
mtukutu katika mazoezi ya klabu yake kwa lengo la kuwafanya
wachezaji wazoe hali ya kuwa wapole wawapo katika uwanja wa Anfield mechi kati ya Manchester United na Liverpool imesha zua kadi
nyekundu 15 katika ligi kuu ya England.

Huku Van Gaal akiwa tayari
amesha shuhudia wachezaji wake wa wili Chris Smalling na Angel Di
Maria wakizawadiwa kadi nyekundu katika mechi kubwa msimu huu
kocha huyo wa Manchester United amekua akiwafanyia majaribio ya
hasira wachezaji wake kwa kufanya maamuzi ya sio sahihi katika
mazoezi kama kuwajenga.Van Gaal alisema
'nimekua refa katika mechi ambazo tumekua tukicheza katika uwanja
wa mazoezi na nimekua nikipiga kipenga katika hali ambayo
wanatakiwa wa kuzuia hasira zao na kuwaandaa na hali ya
uwanja,napia nili watamkia baada ya chakula cha mchana.kuzuia hasira nacho ni kipaji'

Manchester United wamekua na matokeo mabaya katika uwanja wa Anfield hivi karibuni huku ikijikuta imeshinda mechi mechi moja
katika mechi 7,japo Van Gaal hajaishiwa hali ya kujiamini katika
maandalizi ya timu yake huku ikiwa ni mara yake ya kwanza kwenda
katika uwanja wa Anfield kama kocha wa Manchester United

"ni mmoja kati ya viwanja vigumu kwa Manchester United
nimesikia,lakini sasa hivi mimi ndio kocha hapa ya wezekana tukali
badilisha hilo"

0 comments:

Post a Comment