Facebook

Monday 16 March 2015

Mahakama yamuhukumu aliyekuwa mke wa Rais miaka 20 gerezani Ivory Coast.

Mahakama nchini Ivory Coast imemhukumu aliyekuwa mke wa Rais wa
nchi hiyo Laurent Gbagbo, kifungo cha miaka 20 gerezani.

Simone Gbagbo amehukumiwa kifungo hicho baada ya kukutwa na
hatia ya kushiriki katika ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi nchini
humo mwaka 2010 na 2011.

Simone Gbagbo alikamatwa mwaka 2011 pamoja na mume wake,
aliyekuwa rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, ambaye anakabiliwa na
mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya uhalifu
mjini The Hague Uholanzi.
Katika ghasia hizo watu takriban elfu tatu walifariki dunia.

0 comments:

Post a Comment