Facebook

Saturday 21 March 2015

Huduma ya Taxi yapigwa marufuku Ujerumani.

Ni wiki ngumu ya Uber.Mahakama moja nchini Ujerumani imepiga
marufuku huduma ya bei nafuu ya texi ya Uberpop baada ya
kuamua kwamba inaenda kinyume na sheria za uchukuzi.

Vilevile afisi
za kampuni hiyo zilizopo mjini Paris zimevamiwa na maafisa wa polisi
wa Ufaransa wanaochunguza huduma hiyo ya Uberpop,huku watu 30
wanaohusishwa na kampuni hiyo wakishtakiwa kwa kuendesha kampuni
hiyo ya texi nchini Korea Kusini bila vibali.Uber imesema kuwa
wafanyikazi wake wa koreakusini hawajavunja sheria na kuutaja
uvamizi huo wa Paris kama usio wa haki.

0 comments:

Post a Comment