Facebook

Thursday 26 March 2015

FAINALI YA COPA DEL RAY KUCHEZWA NOU CAMP, MADRID YAGOMA KUTOA UWANJA

      Imeamuliwa kuwa Fainali ya Kombe la
Mfalme, Copa del Rey , itachezwa Nou
Camp, Nyumbani kwa Barcelona , hapo Mei
30 kati ya Athletic Bilbao na Barcelona.
          Kawaida Fainali ya Kombe hili huchezwa
Uwanja usio wa Timu iliyo Fainali lakini
baada ya Real Madrid kugomea kutoa
Uwanja wao Santiago Bernabeu ukaanza
mvutano wa wapi Fainali hiyo ichezwe .
         Kwenye Mkutano wa Shirikisho la Soka la
Spain na Klabu hizo mbili , Kura ilitumika na
Viwanja vya Sevilla , Vicente Calderon, na
Mestalla wa Valencia kubwagwa na kuacha
Viwanja vya Barca Nou Camp na San
Mames cha Bilbao kwenye kinyang ' anyiro .
          Hatimae Nou Camp ilipita na hii itakuwa
mara ya kwanza kwa Timu iliyo Fainali
kucheza Fainali Uwanja wake wa
Nyumbani tangu 2002 wakati Deportivo La
Coruna walipoifunga Real Madrid Nyumbani
kwao Santiago Bernabeu .
          Mara ya mwisho kwa Nou Camp kuwa
Mwenyeji wa Fainali za Copa del Rey ni
2010.
          Ikiwa Barca watatwaa Kombe hili , ambalo
wao wanaongoza kwa kulibeba mara
nyingi , hii itakuwa mara yao ya 27 wakati
Athletic Bilbao wakifuata kwa wingi wa
kulitwaa kwa kulichukua mara 23.

0 comments:

Post a Comment