Facebook

Friday 20 March 2015

Roy Hodson atoa ya moyoni kwa kinda Harry Kane.

Kocha wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson amesema
ingeshangaza sana kama mchezaji kinda wa klabu ya Tottenham
Harry Kane asingejumuishwa katika kikosi cha Nchi hiyo
kinachotarajiwa kumenyana na Lithuaniana na Italy.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ni miongoni mwa wachezaji
24 wa kikosi cha England ambacho kimetajwa na Hodgson kucheza
dhidi ya Lithuania mchezo ambao utapigwa katika dimba la Wembley
mnamo march ,27 mwaka huu kwaajili ya mechi za kufuzu katika
mashindano katika mataifa ya Ulaya yanayotarajia kufanyika
mwakani.

Kikosi hicho pia kinatarajia kuumana na Italy katika mchezo
wa kirafiki utakaopigwa mjini Turin huko Italy tarehe 31 mwezi huu.

0 comments:

Post a Comment