Facebook

Saturday 14 March 2015

Unene wamkosesha burudani Uingereza.

Mama mmoja amedai kuwa yeye na marafiki zake wawili walizuiliwa
kuingia katika kilabu moja ya burudani kwa sababu zinazodaiwa kuwa
ni wanene sana na wenye sura mbaya
Stacey Owen 33, alikuwa ametoka na marafiki zake wawili kwa ajili
ya kupata burudani wakati wa usiku siku ya jumamosi alipokataliwa
kuingia katika baa moja jijini Manchester kwa sababu ya unene wake.

Stacey amesema wao walizuiwa huku watu wengine wakiingia katika
baa hiyo maarufu mjini humo,
Klabu ya burudani Uingereza
Mama huyo sasa anataka kuombwa radhi na wamiliki wa Baa hiyo
lakini mpaka sasa amedai hajapata ujumbe wowote kutoka kwao.

Anasema sio kwamba anajiona kwamba yeye ni mrembo sana lakini
kilichomshangaza ni uwepo wa ubaguzi huo miongoni mwa wateja.

0 comments:

Post a Comment