Facebook

Friday 20 March 2015

Mama mjamzito azalishwa bila kupenda baada ya kuchomwa kisu tumboni.

Maafisa wa polisi katika jimbo la Colorado wanasema kuwa mwanamke
mmoja alimdunga kisu mwanamke mjamzito katika tumbo lake na
kumchukua mwanawe ambaye alikuwa hajazaliwa.
Mwathiriwa ambaye alikuwa mja mzito wa miezi saba anatarajiwa
kupona kufuatia upasuaji lakini mtoto aliaga dunia.

Mwanamke huyo mjamzito alikuwa akimtembelea mshukiwa ili
amnunulie mwanawe nguo ambazo zilikuwa zimetangazwa katika katika
soko la mtandao la Craigslist.
Mshukiwa Dynel Catrece Lane alimpoteza mwanawe wa miezi 19
muongo mmoja uliopita alipokufa maji katika kidimbwi cha samaki.

Mwathiriwa mwenye umri wa miaka 26 alikua akitaka kununua nguo
hizo wakati aliposhambuliwa siku ya jumatano.
Wakati alipoingia katika nyumba hiyo alishambuliwa na kupigwa kabla
ya mwanawe kutolewa kutoka tumboni'',Afisa mmoja wa Polisi Jeff
Satur alisema.

Mwathiriwa alifanikiwa kupiga simu ya dharura lakini alipatikana
katika hali mbaya wakati maafisa walipowasili.

0 comments:

Post a Comment