Facebook

Tuesday 3 March 2015

RAIS KIKWETE ASIKIA KILIO CHA ALBINO

"KIKWETE ASIKIA KILIO CHA ALBINO

RAIS Kikwete alisema vitendo vya kinyama ambavyo havitegemewi kufanywa au kutokea katika jamii yoyote iliostarabika, ya watu wanaomwabudu Mungu kujihusisha na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi. 

Rais Kikwete aliyasema hayo  kwenye hotuba yake ya mwishoni mwa mwezi Febuari.

Aidha, Rais Jakaya Kikwete, amesema watu 13 wamehukumiwa kifo na wawili wamepata kifungo cha miezi  sita hadi sasa baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).

Hata hivyo, Rais Kikwete hakueleza watu 13 waliohukumiwa adhabu ya kifo kama wameshanyongwa ama la.

"Jamii ina wajibu wa kuhakisha usalama wa maisha na mali zao kama ilivyo kwa watu wengine wote na kwamba mauji ya albino ni jambo linalofedhehesha na kulizalilisha taifa letu", alisema Rais Kikwete.

Pia alisema Serikali imelipa uzito mkubwa suala la kudhibiti  na kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi."

RAIS Kikwete alisema vitendo vya kinyama ambavyo havitegemewi kufanywa au kutokea katika jamii yoyote iliostarabika, ya watu wanaomwabudu Mungu kujihusisha na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Rais Kikwete aliyasema hayo kwenye hotuba yake ya mwishoni mwa mwezi Febuari.
Aidha, Rais Jakaya Kikwete, amesema watu 13 wamehukumiwa kifo na wawili wamepata kifungo cha miezi sita hadi sasa baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Hata hivyo, Rais Kikwete hakueleza watu 13 waliohukumiwa adhabu ya kifo kama wameshanyongwa ama la.
"Jamii ina wajibu wa kuhakisha usalama wa maisha na mali zao kama ilivyo kwa watu wengine wote na kwamba mauji ya albino ni jambo linalofedhehesha na kulizalilisha taifa letu", alisema Rais Kikwete.
Pia alisema Serikali imelipa uzito mkubwa suala la kudhibiti na kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

0 comments:

Post a Comment