Facebook

Saturday 14 March 2015

Mourinho:Chelsea itashinda ligi kuu Uingereza.

Kilabu ya Chelsea itashinda ligi ya Uingereza,kocha wa kilabu hiyo
Jose Mourinho amebashiri.

The Blues waliondolewa katika mashindano ya kilabu bingwa barani
Ulaya na kilabu ya Parsi St Germain katika mechi ya katikati ya wiki
lakini bado inaongoza jedwali la ligi ya EPL ikiwa na pointi tano huku
ikiwa zimesalia mechi 11.

Mournho:Timu iliong'atuliwa katika mashindano ya kilabu bingwa
barani ulaya ni timu ile ile inayoendelea kuongoza ligi ya Uingereza
tangu siku ya kwanza.

''Ni wachezaji wale wale walioshinda kombe la capital One Cup na
wachezaji haohao ndio watakaoshinda ligi ya EPL''.alisema kocha
huyo.

0 comments:

Post a Comment