Facebook

Tuesday 17 March 2015

Uchambuzi wa mechi kali za Leo LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA Na Mr.CHOI (KWA TAARIFA YAKO)


  AS MONACO vs ARSENAL (3-1)
 

  Baada ya Chelsea,Fc Basel,S.Donesk na Shalke 04 kuondoshwa ktk 16 bora leo na kesho tutashuhudia timu nyingine nne zitazo fungasha vilago.

Waingereza pamoja na mashabiki wengi wa ligi kuu nchini England wakiwa wana amini msimu huu hawata kuwa na timu robo fainal mzee Wenger atabiri kufanya maajabu pale ktk dimba la Louis II.

   Mchezo wa awamu ya kwanza pale Emirates Arsenal walifungwa 3-1 huku Monaco wakiwa na faida ya magoli 3 ya ugenini na kupelekea mchezo huu Arsenal ashinde 3-0 ili apate nafasi ya kutinga robo fainal.

   Ni mchezo ambao una mahesabu magumu sana kwa upande wa Arsenal. Kikosi cha mzee Wenger kinatarajiwa kuwa na Coquelin,  Ramsey na Cazorla dimbani huku Sanchez Giroud na Ozil wakiwa safu ya ushambuliaji safu ya ulinzi Chambers,Mertesacker,Koscielny na Monreal.
 
Upande Monaco ambao pengine wanataka fanya yale ya 2004 kucheza fainal ya Uefa pamoja na Fc Porto walio robo fainal kikosi hakito kuwa na mabadiliko sana kama kile kilicho cheza Emirates. Safu ya kiungo ambayo ilikuwa sumu kwa mzee Wenger itaongozwa na Toulalan,Moutinho na  Kondogbia ambae alikuwa na kiwango bora mbele ya Arsenal safu ya ushambuliaji Silva,Berbatov na Mortal.

  Mpaka sasa Monaco ni miongoni mwa timu zenye safu nzuri ya ulinzi huku wakiwa na asilimia 75% za ushindi michezo ya nyumbani.
    Arsenal hivi sasa wapo ktk kiwango kizuri isipo kuwa kiungo cha chini bado tatizo na wasipo kuwa makini ndoto zao za kuandika historia pale Stade Louis II itakuwa ndoto kwani wanacheza na timu iliyo nzuri sana kwanzia safu ya kiungo hadi ya ulinzi achilia mbali safu ya ushambuliaji.

  Kwa kutafuta ushindi Arsenal watashambulia zaidi ingawa wasipo kuwa makini vijana wa Leonardo Jardims watafanya kama walivyo fanya pale Emirates kwa mashambulizi ya kasi na kushtukiza.
  Ngoja tusubiri  kama historia ita andikwa na mzee Wenger ambaye hajawai ifunga Monaco.
                
**********************************************
 

  A.MADRID vs B.LEVERKUSEN 0-1
Pale katika jiji la Madrid wenyeji A.Madrid watapambana na Bayern Leverkusen walio chini ya Rogers Schmidt.
   Katika mchezo ulifanyika kule Bay Arena goli la Calhanoglu liliwapa B.Leverkusen ushindi wa goli moja kwa bila.

   Kwa hivi sasa timu zote zina viwango tofauti A.Madrid kiwango chao kimeshuka kulingana na matokeo ya hivi karibuni La-Liga na kupelekea kushuka hadi nafasi ya nne huku wapinzani wao wakipanda hadi nafasi nne ktk Bundesliga.
  Kila shabiki ktk dimba la Vicente Calderon ana amini timu yao bado ina uwezo wa kusonga mbele kwenye michuano hii huku vita kubwa itakuwa katika safu ya kiungo licha ya Bender kutokuwepo kwa Leverkusen.

  Simeone atashambulia zaidi kusaka bao licha ya uwezo mdogo wa safu yake ya ushambuliaji kwa siku za hivi karibuni lakini safu yake ya ulinzi isipo kuwa makini na Drmic, Calhanoglu matokeo yatakuwa tofauti na anavyo tarajia.

---------

For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com

0 comments:

Post a Comment