Facebook

Tuesday 25 November 2014

GIROUD NJE LIGI YA MABINGWA ULAYA.

Katika kile kinachoonekana kuwa ndani ya klabu ya Arsenal mambo hayaendi sawa mshambuliaji Mfaransa Olivier Giroud hatoruhusiwa kuitumikia klabu hiyo katika michuano ya Ulaya mpaka hapo Februari mwakani.

Habari iko hivi baada ya Giroud kupata majeruhi na kutangazwa kuwa nje ya dimba kwa miezi mitatu/minne Arsenal ililazimika kulitoa jina la staa huyo katika kikosi chake cha wachezaji 23/25 waliopaswa kushiriki mechi mbalimbali za michuano hiyo yenye utajiri mkubwa katika ngazi ya vilabu.

Hivyo basi kutokana na Giroud kupona mapema kabla ya muda uliotangazwa hatoruhusiwa kucheza michuano hiyo kwakuwa jina lake halimo katika makablasha ya UEFA,mwezi Februari ndipo ataonekana tena dimbani na hii Kama iwapo tu Arsenal itatinga hatua ya mtoano.

0 comments:

Post a Comment