Facebook

Friday 21 November 2014

Yule rais wa kwanza Mzungu Afrika,atimuliwa na Chama chake.

Chama tawala nchini Zambia (PF)
kimemtimua kaimu rais wa nchi hiyo Guys
Scott kutoka chamani na kuvunja utaratibu
wa katiba.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa
chama hicho.
''Amekuwa akiwaajiri na kuwafuta watu kazi
ovyo na pia bila ya kushauriana na kamati kuu
ya chama,'' amesema Malozo Sichone.

Bwana Scott, ambaye licha ya hatua hiyo
ataendelea kuwa mwanachama wa chama
hicho, ataendelea kuhudumu kama kaimu rais
hadi uchaguzi utakapofanyika tarehe 20
Januari.

Scott aliteuliwa kuwa kaimu rais kufuatia kifo
cha hayati Rais Michael Sata aliyefariki mwezi
jana.

0 comments:

Post a Comment