Facebook

Wednesday 19 November 2014

Mmiliki wa 'Club' maarufu Bukoba afariki akiwa anafanya Mapenzi katika Gari lake.


Taarifa tulioipata BantuTz.com  kutoka Bukoba mkoani Kagera ni kwamba.
Mmiliki wa 'Club' maarufu ya LINAS ya mjini Bukoba aitwae Leonard Mtensa Stephen  mwenye miaka 50  hapo jana  [18-11-2014] muda wa saa 4 usiku allifariki maeneo ya Buyekera karibu na 'club' yake ya Linas.

Marehemu alikuwa anafanya mapenzi ndani ya gari lake aina ya IST,Lenye namba za Usajili T.982 CQG na mpenzi wake Jackline Hassan,ambaye ni Mzanaki,mkazi wa Buyekera mwenye miaka 25.
Tulipowasiliana na ripota wetu kutoka Bukoba ametuarifu kwamba Mmiliki huyo wa Club ya Linas kipindi anafanya mapenzi na mpenzi wake huyo ghafla hali ilibadilika na kukimbizwa katika kituo cha Afya cha ELCT Ndolage Manispaa ya Bukoba Mjini ambapo alifia njiani.

Baadaye maaskari walipokuwa wanakagua katika gari lake walikuta vilevi vya aina mbalimbali ikiwemo  Whisky aina ya Bond 7 aliyokuwa anakunywa.
 
Mpenzi wake Jackline Hassan anashikiliwa na  Jeshi la Polisi hadi hivi sasa ili kusaidia upepelezi.

Hadi hivi sasa chanzo cha kifo chake hakijajulikana.
Tutakujuza kila kitakachokuwa kinaendelea kuhusiana na sakata hili.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata taarifa zote mbalimbali kutoka kila kona ya dunia kwa wakati na muda muafaka.

0 comments:

Post a Comment