Facebook

Tuesday 25 November 2014

Silaa aeleza sababu ya kuendesha Oparesheni 'delete CCM'

Katibu mkuu wa CHADEMA
Dk.Wilbroad Slaa ametaja baadhi ya sababu za
chama hicho kuendesha operesheni maalumu
inayojulikana kama ‘delete CCM’ katika mikoa
saba hapa nchini.

Akihutubia wananchi wa kijiji cha Kwermusl
Wilayani Mbulu mahali alikozaliwa, katibu mkuu
huyo wa chadema Dk.Wilbroad Slaa amesema
operesheni hiyo iliyoanza novemba 5 mwaka
huu lengo lake ni kuiondoa CCM madarakani
kufuatia baadhi ya viongozi wa serikali ya chama
cha mapinduzi kuweka mbele maslahi yao
binafsi na kushindwa kuwatumikia wananchi
ambao kwa zaidi ya miaka 50 ya Uhuru
wameendelea kuishi katika lindi la umaskini
uliotopea.

0 comments:

Post a Comment