Facebook

Friday 21 November 2014

Kifo cha Mtoto mchanga chazua tafrani Uganda.

Shughuli za mazishi ya mtoto wa miaka
miwili zimefanyika nchini Uganda, mtoto
ambaye kifo chake kimezua ghadhabu
baada ya mtoto huyo kugongwa na gari la
halmashauri ya jiji la Kampala ,baada ya
mama yake kukamatwa akiuza matunda
kinyume cha sheria.
Familia ya Ryan Ssemaganda na wanasiasa wa
upinzani walitishia kutomzika mtoto huyo
mpaka maofisa hao watakapo wajibika kwa
kitendo hicho.Mwili wake ulichukuliwa wakati
wakiandamana kuelekea bungeni siku ya
alhamisi.
Raia wa Uganda wanaona kuwa halmashauri
hiyo inatumia nguvu nyingi kupambana na
wachuuzi wa mitaani.

Mama wa mtoto Ryan alikamatwa siku ya
jumatatu baada ya kukutwa akiuza matunda
huku akiwa hana leseni.
Siku iliyofuata, Bibi wa mtoto huyo alimpeleka
katika Ofisi za Mamlaka ya mji wa Kampala
ambako mama mtoto alikuwa akishiliwa , nia
ilikua kumpa mama mtoto ili amnyonyeshe.

Maafisa wa Ofisi hiyo walikataa na wakati
wakijadiliana kuhusu hilo, mtoto alichoropoka
kutoka kwa mama yake na kugongwa na gari
linalomilikiwa na Mamlaka hiyo.
Siku ya Alhamisi polisi ilizuia kupelekwa kwa
mwili katika Bunge, wakisisitiza mwili huo
uzikwe ili marehemu apumzike kwa amani, na
kuwataka waepuka jambo hilo kushughulikiwa
kisiasa.

0 comments:

Post a Comment