Facebook

Monday 24 November 2014

MDAHALO WA KATIBA ULIOKUWA UFANYIKE NOV 25 MLIMANI CITY UMEHAIRISHWA TENA

Taarifa rasmi zinasema kuwa vyombo vya
usalama na hasa jeshi la polisi wameuzuia
mdahalo huo kwa sasa kutokana na ile
kinachodaiwa kuwapo taarifa za vijana
waliopanga kuandamana kuvuruga na kuzuia
mdahalo huo wakidai kuwa wajumbe hao
wabunge la katiba wanatumika kufunika mjadala
wa pesa za escrow na kuwapo madai kuwa
Lugemalila aliichangia taasisi ya Mwalimu
Nyerere shilingi milioni mia tano,vijana hao
ambao waliandika barua na kuitupa makao
makuu ya polisi DSM, wamelitaka jeshi la polisi
kuzuia mdahalo huo kwa sasa hadi sakata la
escrow akaunti litakapo jadiliwa vinginevyo
watafanya kila wawezalo kuvuruga amani
mlimani city
taarifa zinasema pia kuwa viongozi wa taasisi
ya mwalimu nyerere bado wanafanya juhudi
mbalimbali kuhakikisha kila kijana atakaeshiriki
mdahalo huo anapekuliwa na kujulikana na
camera zilizopo maeneo hayo ya mlimani city
pamoja na kuongeza ulinzi wa kampuni
binafsi ,maombi hayo yanasubiria kikao cha
kesho cha jeshi la polisi na uongozi wa taasisi
ya mwalimu nyerere na washiriki wengine wa
mdahalo ili maafikiano yao yatolewe rasmi ni lini
mdahalo huo umepangwa baada ya kusogezwa
mbele toka NOV 25 siku ya jumanne

0 comments:

Post a Comment