Facebook

Wednesday 19 November 2014

Vurugu kati ya Askari na Wamachinga zatokea Mwanza ,Askari Mmoja apoteza Maisha.

Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka kwa ripota wetu  Jijini Mwanza ni kwamba:-

Kumotokea vurugu kubwa katikati ua Jiji la Mwanza.

Vurugu hizo zilianza mida ya saa saba mchana baada ya Mgambo kuwafukuza Wamachinga eneo la Msikiti wa Wahindi  lakini wamachinga hao walikataa kuondoka.Vurugu zikaanza kati ya Mgambo na Wamachinga. Wamachinga waliwazidi Nguvu mgambo.

Machinga  walivamia na kubomoa vioo vya msikiti wa wahìndi huku Mgambo mmoja katika purukushani alianguka chini baada ya kupigwa na vioo,alivamiwa na kupigwa hadi kufa papo hapo na Wamachinga.Huku Magambo wengine  6 wakijeruhiwa vibaya.

Baada ya mgambo kuzidiwa nguvu,Polisi walikuja kutuliza ghasia jambo ambalo hawakufanikiwa
Waliamua kuridi ili waongeze nguvu ndipo mgambo walipopata mwanya wa kupasua vioo vya msikiti huo wa wahindi uliojengwa kwa gharama kubwa sana kwa kutumia mawe.

Wamachinga hawakuishia hapo kwani walivamia magari matatu ya wahindi wanaoswali katika msikiti huo na kupasua vioo vya magari hayo Land Cruiser mbili na Toyota Corrola moja

Kwa bahati mbaya,jinsi uhuru wa habari unavyokandamizwa Hakuna picha yoyote iliyopigwa na wale waliokuwa wanapiga picha wamekamatwa na askari wa kikosi cha Kutiza Ghasia FFU.

Hadi Jioni ya leo Askari wa kutuliza Ghasia walikuwa wametapakaa katika eneo la tukio na kufunga barabara kwa usalama wa mali za wafanyabiashara.

Endelea kutembelea www.bantutz.com tutakuletea kila kitakachokuwa kinajiri kutoka Jijini Mwanza.

0 comments:

Post a Comment