Facebook

Monday 24 November 2014

Serikali ya mpito Burukina Faso kukutana leo kwa mara ya kwanza.

Serikali mpya ya mpito nchini Burkina Faso itakuwa na mkutano wake wa kwanza leo hii huku jeshi likishikilia nyadhifa muhimu wiki tatu baada ya kuchukuwa madaraka kufuatia kun'gatuka kwa rais wa nchi hiyo kutokana na uasi wa umma.

Kiongozi mwenye nguvu jeshini Luteni Isaac Zida ataendelea kushikilia wadhifa wa waziri mkuu na waziri wa ulinzi. Katibu mkuu wa serikali hiyo mpya Alain Thierry Ouattara ametangaza kwamba jeshi pia litadhibiti wizara ya ulinzi.
Kwa jumla maafisa wanne wa jeshi wamejumuishwa katika baraza la mawaziri lenye mawaziri 26 ambapo Rais Michel Kafando atashikilia pia wadhifa wa waziri wa mambo ya nje. Jeshi limeahidi kuirudisha nchi hiyo kwenye utawala kamili wa kiraia.

0 comments:

Post a Comment