Facebook

Tuesday 18 November 2014

Bwana harusi ampa talala Bibi harusi siku ya Kufunga Ndoa.

Bwana harusi mmoja kutoka Saudi Arabia
amempa talaka mkewe siku ya harusi
baada ya kumuona uso wake kwa mara ya
kwanza wakati mpiga picha alipotaka
kuwapiga picha.

Maharusi hao kutoka mji wa magharibi wa
Saudia,Medinah walikubaliana kuoana licha ya
kutoonana uso kwa uso,swala ambalo ni
utamaduni mkubwa wa mataifa ya mashariki ya
kati.

lakini wakati mwanamke huyo alipofungua
kitambara alichokuwa amejifunika uso na
kutabasamu katika kamera,mumewe alishtuka
na kuondoka wa ghafla.
Kulingana na gazeti moja katika eneo hilo kwa
jina Okaz,mwanamume huyo alianguka na
kuzirai huku wageni waalikwa wakijaribu
kuingilia kati ili kutatua kilichokuwa
kikiendelea.

Hatahivyo Bwana harusi alisema kuwa
hakuweza kumwona bi harusi kabla ya harusi
yao gazeti hilo la Okaz liliripoti.

'' Si wewe msichana niliyetaka kuoa,si wewe
kamwe niliyedhani,kwa hivyo nakupa
talaka''
alisema bwana harusi.
Na alipompa talaka bi harusi naye alianguka na
kuzirai na kuifanya harusi hiyo kuwa usiku wa
majonzi.

Chanzo:BBC

0 comments:

Post a Comment