Facebook

Thursday 20 November 2014

Binti akataa kuasiliwa na Kim Kardashian Thailand.

Mtoto aliyekuwa akiishi katika mazingira ya
umasikini katika Nyumba ya kulea Watoto
yatima nchini Thailand amefanya uamuzi
wa kushangaza alipokataa ombi la Nyota
maarufu duniani Kim Kardashian kumuasili
kuwa sehemu ya familia yake.

Taarifa zinasema binti huyo alifurahi sana
aliposikia milionea huyo anataka kumuasili,
lakini alisisitiza kuwa anataka kusoma nchini
Thailand akimtaka Kim kuisaidia nchi yake na
watoto wenzake wanaoishi pamoja katika
nyumba ya watoto yatima.

Kim alivutiwa na binti huyu aitwae Pink
mwenye umri wa miaka 13, alipotembelea
nyumba ya watoto yatima katika Jimbo la
Phang Nga,eneo ambalo zaidi ya watu 4,000
walipoteza maisha kutokana na Tsunami mwaka
2004.

Pink alipelekwa na mama yake katika nyumba
ya kulelea watoto kwa kuwa hakuweza kumlea
mtoto huyo na kugharamia elimu yake.
Binti huyu anasema yeye na Watoto wenzake
walipokutana na Kim Kardashian
hawakumfahamu yeye ni nani.

Pink ambaye jina lake halisi ni Laddawan Tong-
Keaw, alifurahi kukutana na Nyota huyo,
amesema na yeye anapenda sana kuonekana
kwenye Televisheni.

Pink husafiri umbali wa Maili 100 kwa basi na
Watoto wenzake wawili kwenda Shule
inayoongoza jimboni humo inayomilikiwa na
Serikali baada ya kufaulu mitihani yao kuingia
shule hiyo.
Binti huyu huamka saa kumi na moja alfajiri
na kurejea nyumbani saa kumi na mbili jioni.

0 comments:

Post a Comment